Na Matukio Daima media
Mwanaharakati wa haki za binadamu na wakili mashuhuri nchini Tanzania, Laetitia Petro Ntagazwa, ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) ameshika nafasi ya 34 na kuweza kutambuliwa na kuingia katika orodha ya wanawake 100 wenye ushawishi mkubwa barani Afrika wanaotumia sheria kusaidia jamii na kuwa na mchango mkubwa kwa wanawake katika sekta ya sheria na maendeleo ya jamii.
Kulingana na ripoti iliyotolewa na Courtroom Mail 100 ya tarehe 2 Aprili mwaka huu wa 2025 Makamu huyo wa Rais wa (TLS) ameshika nafasi ya 34 katika orodha hiyo. Hii ni kutokana na kazi yake ya kujitolea katika kutoa msaada wa kisheria kwa watu wasio na uwezo, kupigania haki za binadamu, na kukuza usawa wa kijinsia katika jamii.
Akizungumza na Matukio Daima Tv Ntagazwa amesema kuwa anafurahishwa kwa kutambuliwa kwa kazi yake na kwamba hii itamchochea kuendelea kufanya kazi kwa bidii zaidi na ataendelea kufanya kazi ya kutetea jamii huku akitoa shukrani zake za dhati kwa jamii.
"Ninawashukuru sana wanajamii Pamoja na wanahabari kwasababu hizi kazi za kisheria za kujitolea zinahitaji sana kupata usaidizi wa vyombo vya habari ili kuweza kutambulika lakini katika harakati za kusaidia jamii hii ni kazi yetu sote na ni heshima kubwa kwangu kupokea tuzo hii kutoka kwa jarida lenye heshima kama Courtroom Mail na ninapenda kutumia fursa hii kuwashukuru wote ambao wanashirikiana na sisi katika kusaidia jamii.
Pia Ntagazwa ameeleza faida ya nafasi hiyo aliyoipata katika kuendelea kusaidia jamii katika hatua mbalimbli za kisheria pia ameeleza umuhimu wa wanawake wanasheria na kina mama kuweza kutambua thamani zao katika jamii na Tanzania kwa ujumla.
"Kwanza niendelee kuzishukuru Taasisi mbalimbali ambazo zimeendelea kuwa Pamoja nami na katika hili niseme nimepata hamasa kubwa zaidi ya kuweza kuendelea kutetea haki za wanajamii katika nchi yetu na kwa upande wa wanawake niendelee kuwatia moyo katika kazi zao ambazo wanafanya za kusaidia jamii na pia hamasa hii itaniwezesha kusimama katika kuhakikisha kuwa thamani na wajibu wao unatambulika katika jamii na bara zima la Afrika.
Mbali na kutambuliwa kwa mchango wake binafsi.
Ntagazwa pia ameelezea umuhimu wa mipango ya usaidizi wa kisheria inayoendeshwa na serikali, hasa ile inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan akielezea jinsi mipango hiyo ilivyokuwa na mchango mkubwa katika kuwafikia wananchi wasio na uwezo na kuwapatia haki zao.
“Naipongeza sana serikali kupitia wizara ya Katiba na sheria kwa kuja na kampeni maalumu ya Mama Samia Legal Aid Clinic ambayo kimsingi imehasisiwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na katika jamii zetu changamoto kubwa ambazo zimeonekana ni masuala ya migogoro ya ardhi,ukatili wa kijinsia na masuala ya ndoa na niseme tu mipango hii ya usaidizi wa kisheria ni muhimu sana katika kujenga jamii yenye usawa na haki na Tunahitaji kuendelea kuiunga mkono na kuhakikisha inawafikia wale wote wanaohitaji"
Laetitia Petro Ntagazwa ni wakili wa Mahakama Kuu na mahakama nyingine za chini Yeye ndiye mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Sauti ya Haki Tanzania (SHTZ). Pia ni Makamu wa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), mwanzilishi na Mjumbe wa Bodi ya Muungano wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania, mwenyekiti wa Kamati ya Watoa Msaada wa Kisheria Mkoa wa Mbeya, mwanzilishi na Mwenyekiti wa Wakili Welfare Mkoba, mwanzilishi na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Jinsia na Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania, Mwenyekiti wa Chuo cha Ualimu cha Rungwe na Mwenyekiti wa Chuo cha Ualimu cha Rungwe, Wakili Welfare Mkoba. Kamati ya Maadili ya Mahakimu wa Msingi.
0 Comments