Header Ads Widget

UJENZI MIUNDO MBINU KIGOMA KUIMARISHA BIASHARA YA KIMATAIFA





Na Fadhili Abdallah,Kigoma

WAZIRI wa nchii ofisi ya Raisi Ikulu Kazi Maalum George Mkuchika amesema kuwa serikali imedhamiria kutekeleza na kukamilisha miradi yote ya miundo mbinu mkoani Kigoma ili kuongeza shughuli za kiuchumi na biashara baina ya  Tanzania na nchi za Ukanda wa maziwa makuu.

Waziri Mkuchika alisema hayo Manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani Kigoma akianza ziara ya siku nne mkoani humo kutembelea miradi na ...kufanya mikutano ya hadhara na wananchi kueleza kazi kubwa inayofanywa na serikali ya Raisi Samia Suluhu Hassan katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya wananchi.

Katika ziara hiyo Waziri Mkuchika ametembelea mradi wa maboresho na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Kigoma, kutembelea bandari ya Kigoma na kukagua utekelezaji wa miradi ya ukarabati wa meli za Mv.Liemba na MT Sangara na kusema kuwa miradi yote ambayo serikali inatekeleza itakamilishwa.





Alisema kuwa serikali kwa sasa iko katika utekelezaji wa reli iendayo kasi (SGR) kutoka Tabora kupitia Uvinza mkoani Kigoma kwenda Msongati nchini Burundi ambapo baada ya hapo reli hiyo itaenda Gitega mji Mkuu wa Burundi na kwenda Lubumbashi nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).

Waziri huyo alisema kuwa kwa sasa ndege za Shirika la Ndege (ATCL) zinafanya safari zake kutoka Dar es Salaam kupitia Kigoma hadi Bujumbura mara tatu kwa wiki na hiyo yote inawezesha wananchi wa nchi hizo mbili kusafiri bila kuzuizi wala shida zozote na kufanya kuwa na mwingiliano mkubwa wa shughuli za biashara na kijamii baina ya nchi hizo.

Awali Akitoa taarifa kwa Waziri Mkuchika Meneja wa Wakala wa barabara  (TANROADS) mkoa Kigoma,Narcis Choma alisema kuwa Mradi wa uboreshaji wa uwanja wa ndege wa Kigoma utahusisha jengo la kuondokea na kufikia abiria, ujenzi wa uzio wa uwanja, mnara wa kuongozea ndege na taa katika barabara za kuongozea ndege.



Choma alisema kuwa mradi huo utagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 46.6 chini ya kampuni ya China Railways Engineering ukiwa mradi wa miezi 18  na kwamba kukamilika kwa mradi huo kutaongeza idadi ya abiria wanaotumia uwanja wa ndege wa Kigoma  kufikia 400,000 kutoka chini ya 100,000 wanaosafiria kupitia uwanja huo.

Akizungumza kwenye ziaraa hiyo Mkuu wa mkoa Kigoma,Thobias Andengenye alisema kuwa kwa miaka minne taangu Raisi Samia aingie madarakani mkoa Kigoma umepatiwa kiasi cha shilingi Trilioni 11.9 ambazo zinatekeleza miradi mbalimbali ikiwemo hiyo ya miundo mbinu ya usafiri na usafirishaji.

Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI