Header Ads Widget

MACHUNGU YA USHURU MPYA WA TRUMP YAANZA KUONEKANA KWENYE MASOKO YA HISA YA KIMATAIFA




 Masoko ya hisa nchini Marekani yamehitimisha wiki yao mbaya zaidi tangu 2020, huku viwango vikubwa vya ushuru wa Donald Trump vikiendelea kusababisha taharuki kwenye masoko ya kimataifa.

Viashiria vyote vikuu vya Wall Street vimeanguka kwa zaidi ya 5%. Trump, kwa upande mwingine, amesisitiza tena kwamba ushuru kwa bidhaa zinazoingia Marekani uta ‘’imarisha" uchumi wa Marekani.

Baadhi ya ushuru sasa umeanza kutumika - na "bei ya msingi" ya 10% ikipitumika kwa bidhaa kutoka Uingereza na mataifa mengine mengi.

Hayo yanajiri wakati huu kampuni ya kemikali Uingereza ikisema ushuru unaweza kuzuia washindani wa bei nafuu. Kemikali za asili ni moja ya bidhaa kubwa zinazoingizwa kutoka Uingereza hadi Marekani, zikiambatana na jumla ya karibu £3 bilioni kwa mwaka jana.

Kemikali hizi hutumika katika sekta mbalimbali kubwa, kuanzia kwenye chakula hadi vipodozi, injini, na kilimo. Badala ya kuhofia ushuru wa Marekani, kampuni ya Robinsons Brothers inadhani kuwa huenda ushuru huu ukasaidia kampuni ya kemikali za asili kurejesha wateja wa Marekani kutoka kwa washindani wa bei nafuu kutoka nje ya nchi.

Chini ya utawala mpya wa Trump, bidhaa kutoka China zitakabiliwa na ushuru wa 34%, wakati bidhaa kutoka India zitatozwa ushuru wa 27%.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI