Header Ads Widget

"DR JANABI ANAWEZA KUSHINDA KWA ZAIDI YA ASILIMIA 70" - YERICKO NYERERE


Na. Andrew Chale,

Mwanasiasa na Mwandishi nguli wa vitabu ambaye pia ni Mwanaharakati Yericko Nyerere ametoa utabiri wake juu ya Mgombea wa Tanzania katika nafasi ya WHO Afrika, inayogombewa na Profesa Janabi.

Yericko Nyerere katika ukurasa wake ameelezea kuwa Prof Janabi ananafasi kubwa ya  ushindi, kwani anaamini Mataifa kadhaa yatamuunga mkono.

Ameandika:

"Mgombea wa Ukuu wa Shirika la Afya Kanda ya Afrika Profesa Janabi @prof.janabi amefika Ikulu ya Bukinabe mbele ya Rais wa nchi hiyo Kapten Ibrahim Traore kuomba kura na kuomba kuungwa mkono kwa mataifa yaliyounda ukanda mpya wa Sahel Magharibi (The Alliance of Sahel States (AES) chini ya Mali, Niger, na Burkina Faso


Kijiographia Janabi anaonekana atashinda, ukizingatia washindani wake wa Wanatoka kanda moja ya Afrika Magharibi ambao ni Ivor Cost, Guinea, Togo, Kitendo kinachotafsirika kuwa hawa watagawana kura za kanda hiyo, huku Janabi akiungwa mkono na Afrika Mashariki yenye nchi 7 isipokuwa moja tu, Janabi anaungwa mkono na nchi za SADC karibu zote isipokuwa mbili kura zao zina utata.

Janabi ana uhakika wa kuvuna robo ya kura ukanda wa Kaskazini mwa Afrika kwa kutumia historia nchi yetu na historia ya Uchaguzi wa Hayati Dr Faustine Ndugulile, lakini pia nchi za ukanda wa Ikweta napo ataokota kura nyingi. 

Kampeni za Janabi zinaongozwa na mtaalamu ww mikakati na diplomasia Rais Mstaafu Jakaya Kikwete. Utabiri unaweza kuwa wa ushindi wa 70%+ 

Na Yericko Nyerere



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI