Na Mwandishi Wetu-Musoma
TIMU ya FFU Mara wameibuka mabingwa wa bonanza la kuadhimisha miaka 61 ya Muungano lililofanyika kwenye uwanja wa Posta mjini Musoma.
Ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Biashara United Veteran umetosha kuwapa ubingwa vijana wa kutuliza ghasia na kutangazwa mabingwa na kupata zawadi ya shilingi 80,,000.
Kocha wa timu ya FFU Mara Coplo. Mzamiru Idrisa amekipongeza kikosi chake kwa kupambana na kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo.
Amesema siri kubwa ya ushindi ni kuzingatia maelekezo yake na hiyo ndio sababu ya kushinda kwa mabonanza mbalimbali yanayoandaliwa.
Kocha huyo ameseema licha ushindi huo taasisi mbalimbali zinapaswa kushiriki ili kuhamsha ari ya michezo mjini Musoma na kuacha kujiweka pembeni na kudai wapo kwenye maandalizi ya kutoka kwaajili ya michezo ya kujenga mahusiano.
Nahodha wa timu hiyo Baraka Mfungo amesema mchezo ulikuwa mgumu dhidi ya wapinzani wao lakini pumzi na kufuata maelekezo kumewapa ushindi.
Amani Kapama mmoja wa wachezaji wa Biashara United Veteran amesema wamepoteza mchezo huo na kocha wao atakwenda kuona walipokosea ili aweze kurekebisha.
Mratibu wa Bonanza hilo Shomari Binda amesema licha ya bonanza kulenga kusherehekea miaka 61 ya Muungano lakini pia linajenga mahusiano.
Amesema polisi na wananchi wanapaswa kuwa na urafiki ikiwa ni pamoja kwa kupitia michezo na kuwaomba wadau mbalimbali kuandaa matukio ya michezo ili kukutana.
MWISHO
0 Comments