Nchi hii Watu wengi sana wanachukia haki za binadamu hadi kuna muda najiuliza hawa wenzetu ni binadamu au pengine ni wanyama wenye sura za binadamu? manake haingii akilini kumwona binadamu akizichukia haki zake mwenyewe.
Watu wanasahau kuwa hata Mwalimu Nyerere alitumia mising hii y’a haki za binadamu kudai uhuru wetu. Watu wanasahau kila unachofanya toka asubuhi hadi unalala ni haki za binadamu.
Kwenda shule ni haki za binadamu, Matibabu ni haki , Kula ni haki , kuongea ni haki , kufanya kazi ni haki ,kutembea ni haki , Kuishi kwa mila na tamaduni zako ni haki za binadamu , kusali ni haki , kuchagua na kuchaguliwa ni haki , kujumuika ni haki, kumiliki mali ni haki, ulinzi na usalama ni haki, ulinzi dhidi ya ukatili wa watoto ni haki, kwa ufupi kila kitu ni haki.
Sasa nashangaa hawa binadamu wenzangu wao kwanini wachukuie haki za binadamu. Wakili Olengurumwa Olengurumwa-March 2025
0 Comments