Header Ads Widget

WANANCHI WAASWA KUYALINDA MAENDELEO YA RAIS DK. SAMIA.

Katibu wa Itikadi, Uenezi, Siasa na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), CPA Amos Makala, kwenye maadhimisho ya Miaka 4 ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan yaliyofanyika uwanja wa CCM mjini Bariadi.
 


Na COSTANTINE MATHIAS, Simiyu.


WANANCHI katika maeneo mbalimbali nchini wametakiwa kuyalinda maendeleo yaliyoletwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ambaye ameliheshimisha Taifa kwa kuwaletea wananchi Maendeleo. 


Aidha, imeelezwa kuwa Tanzania imeendelea kubaki kisiwa cha amani na kwamba nchi jirani zimekuwa zikitumia nchi yetu kama darasa ambapo Amiri Jeshi Mkuu ameendelea kulinda amani hiyo.


Hayo yamebainishwa leo, March 22, 2025, Mkoani Simiyu na Katibu wa Itikadi, Uenezi, Siasa na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), CPA Amos Makala, kwenye maadhimisho ya Miaka 4 ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan yaliyofanyika uwanja wa CCM mjini Bariadi.



Makala amesema kuwa kuna baadhi ya watu wanakejeli na kubeza miaka minne ya Dk.Samia, hivyo wananchi wanatakiwa kuwaonyesha miradi Maji, Afya, Elimu na Umeme ambayo imetekelezwa katika maeneo mbalimbali huku akiwaasa kudumisha amani, Umoja na mshikamano ili waendelee kushuhudia Maendeleo mengi zaidi.


"Tudumishe Amani, Umoja na Mshikamano ili tuendelee kushuhudia Maendeleo mengi zaidi, mwaka huu tunaenda katika Uchaguzi hivyo tutawaletea Wagombea wa Ubunge na Udiwani wanaokubalika kwa wananchi" amesema Makala.


Amesema CCM itaendelea kusimamia serikali yake ili Uchaguzi ukiisha nchi ya Tanzania iendelee kubaki salama na Watu wake.


Katika hatua nyingine Makala ameppngeza ushirikiano uliopo baina ya Chama na Serikali katika Mkoa wa Simiyu ambapo miradi mingi ya Maendeleo inasimamiwa vizuri.



Mwenyekiti CCM Mkoa wa Simiyu, Shemsa Mohammed amesema kuna Ushirikiano ni mkubwa baina ya Chama na serikali hali inavyofanya Usimamizi na Utekelezaji wa miradi kuwa mzuri. 


"Kuna ushirikiano Mkubwa kati ya Chama na serikali, ndio maana Kuna Maendeleo makubwa kwenye Utekelezaji miradi ya Maendeleo, tufikishie salama kwa Rais...tunamwomba aje kutembelea na kuona miradi aliyotekeleza" amesema Shemsa.


Awali Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Kenani Kihongosi amesema ndani ya miaka minne ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, miradi mbalimbali yenye thamani ya shilingi Bil. 840 imetekelezwa katika sekta za Afya, Elimu, Maji, Umeme, Barabara, na miundombinu mingine.


Mwisho.


Katibu wa Itikadi, Uenezi, Siasa na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), CPA Amos Makala (mwenye skafu shingoni), akimsikiliza Afisa Tehama wa CCM Mkoa wa Simiyu Mayala Elias namna anavyosajili wanaCCM kielektroniki.


MKUU wa Mkoa wa Simiyu, Kenani Kihongosi (kushoto) akiwa na Katibu wa Itikadi, Uenezi, Siasa na Mafunzo wa CCM, CPA Amos Makala kwenye maadhimisho ya Miaka 4 ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.


Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Shemsa Mohammed akiongea na Wananchi wa Mkoa wa Simiyu kwenye maadhimisho ya Miaka minne ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, yaliyofanyika uwanja wa CCM mjini Bariadi.


Wananchi na Wana CCM wakiwa kwenye maadhimisho ya Miaka 4 ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan, yaliyofanyika uwanja wa CCM mjini Bariadi.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI