Timu ya Soka ya Kajuna FC ya mkoa Kigoma.
Na Fadhili Abdallah, Kigoma
LICHA kubanwa na kutoka suluhu ya bila kufunga katika mechi yake ya tano ya ligi ya mabingwa wa mikoa kituo cha Kigoma timu ya soka ya Kajuna FC ya mkoa Kigoma imejihakikishia kucheza robo fainali ya ligi ya mabingwa ya mikoa.
Matumaini hayo yanakuja baada ya timu hiyo kufikisha poiti 13 baada ya kucheza michezo mitano kati ya sita inayotakiwa kucheza ikiwa inaongoza kituo cha Kigoma ambapo ni timu ya Igunga ya mkoani Tabora yenye pointi 10 ikiwa imecheza michezo minne na kubakisha michezi miwili ndiyo inayoweza kuifikia timu hiyo ya Kigoma.
Katika mchezo wake wa tano dhidi ya timu ya Dew Drop ya mkoa Sumbawanga uliofanyika kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma timu ya Kajuna ilishindwa kupata ushindi na hivyo kutoka suluhu ya bila kufungana na hivyo kutia doa ushindi mfululizo wa mechi zake nne ilizocheza awali.
Kwa sasa kwa matokeo hayo Kajuna ina uhakika wa wa kucheza robo fainali baada ya kukusanya pointi 13 ikibakisha mchezo mmoja ikifuatiwa na timu ya Igunga ya Tabora yenye point 10 iliyobakisha michezo miwili hivyo kuweza kufikisha pointi 16 ikiwa timu pekee itakayoungana na timu ya Kajuna kucheza robo fainali.
Aidha timu ya Home Boys ya Katavi inashika nafasi ya tatu kwa kuwa na point saba ikiwa imecheza michezo mitano hivyo iwapo itashinda mchezo wake wa mwisho inaweza kufikisha point 10 ambazo tayari timu zinazoongoza zimeshazifikia
Timu ya kyela FC ya Mbeya inashika nafasi ya nne kwa kuwa na pointi sita baada ya kucheza michezo minne ikiwa imefungana pointi Timu ya The Green ambayo pia ina pointi huku timu ya Dew Drop ya Sumbawanga ikiwa na point moja na timu ya Magic Pressure na Singida ikiwa haina pointi baada ya kucheza michezo minne.
Mwisho.
Waamuzi waliochezesha mchezo kati ya Kajuna FC ya Kigoma na Dew Drop ya Sumbawanga mkoa Rukwa ambazo zilitoka Suluhu kwenye mashindano ya Ligi ya mabingwa wa mikoa kituo cha Kigoma.
0 Comments