Na Fadhili Abdallah,Kigoma
WAUMINI wa dini ya kiislam mkoani Kigoma wametakiwa kutumia mafundisho yaliyokuwa yanatolewa katika mwezi mtukufu wa Ramadhani katika kumcha Mungu na kutenda mema kuwa ndiyo tabia na maisha yao ya kila siku ili kuifanya dunia kuwa sehemu nzuri na salama ya kuishi.
Hassan Kiburwa Shekhe wa mkoa Kigoma
Shekhe wa mkoa Kigoma, Hassan Kiburwa amesema hayo katika mawaidha ya Sala ya Eid El fitr iliyofanyika kimkoa katika viwanja vya Kawawa Ujiji mjini Kigoma ambapo amewataka Watanzania kuishi kama ndugu kwa Amani na kupenda na kuacha na mambo yanayosababisha Amani kuvunjika.
Shekhe Kiburwa alisema kuwa mwezi mzima wa Ramadhani waumini ambao walikuwa wamefunga kwa kufuata mafundisho ya dini na Sunna za Mtume Muhamad (SAW) walikuwa wakifanya matendo yeye tabia njema na kuondokana na maasi hivyo ametaka mambo hayo yawe sehemu ya maisha ya watu hao na siyo kuondoka kwa mwezi wa Ramadhani kufanye warudi kwenye kufanya matendo mabaya.
Katika salam kwa waumin na wananchi wa mkoa Kigoma Shekhe huyo wa mkoa Kigoma amewataka Watanzania kumuombea dua njema Raisi wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan na wasaidizi awe na afya njema aweze kutekeleza vyema jukumu lake la kuwatumikia watanzania.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya Kigoma, Rashid Chuachua alisema kuwa kwa mwezi mzima wa Ramadhani wilaya hiyo na sehemu kubwa ya mkoa ilikuwa Amani na usalama idadi kubwa ya watu wakifanya matendo ya kumpendeza Mungu kwa kufuata mafundisho ya dini zao kwa waislam na wakristu ambao walikuwa kwenye mfungo kwa pamoja na kwamba ametaka mambo hayo yawe sehemu ya maisha ya Watanzania.
Shekhe Mustapha Khalfan Kiumbe Mwenyekiti wa Istiqama Foundation mkoa Kigoma
Akiongea kwenye sala ya Eid El Fitr kwenye viwanja vya Kawawa Ujiji Kiongozi wa Taasisi ya ISUWAT mkoa Kigoma, Dabas Khalfan Kiumbe aliwataka Waumin wa kiislam na watanzania wote kuishi kwa upendo kufuata mafundisho ya dini ili kuachana na mambo yanayomchukiza Mungu.
Shekhe Dabas Khalfan Kiumbe Kiongozi wa Taasisi ya ISUWAT mkoa KigomaAwali Mwenyekiti wa Taasisi ya Istiqama Foundation, Mustapha Khalfan Kiumbe alisema kuwa kitendo cha waumin wa kiislam kusali Eid kwa siku tofauti ni utengano mkubwa kwa waislam ambao wanapaswa kuunga na kuwa kitu kimoja badala ya kuwatengeneza kwa kufuata tifauti za kidunia zinazopingana na maandiko ya dini.
Mwisho
0 Comments