Na Shomari Binda-Musoma
MKUU wa Wilaya ÿa Musoma Juma Chikoka amezungumzia suala la umuhimu wa amani na jamii kushirikiana.
Kauli hiyo ameitoa leo machi 31,2025 kwenye Msikiti mkuu wa Ijumaa mjini Musoma baada ya kumalizika kwa swala ya Eid.
Amesema suala la amani lina umuhimu mkubwa kwenye taifa na kuwaomba waumini ya Dini ya Kiislam kuendelea kuiombea amani ya nchi wakati wote.
Chikoka amesema amani na upendo ambao umekuwepo kwenye kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhan inapaswa kuendelea katika kipindi cha miezi mingine.
Amesema katika kipindi cha mfungo unyenyekevu ulikuwa mkubwa kwa waumini na kudai yale yaliyokuwa takihubiliwa na ma Sheikh misikitini yanapaswa kuzingatiwa kwa kipindi chote.
" Tupo kwenye sherehe ya Eid baada ya kumalizika kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa waumini wa Dini ya Kiislam.
Katika swala hiyo ya Eid Sheikh wa mkoa wa Mara Msabaha Kassim amewaongoza waumini wa dini ya Kiislam kumuombea Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan na taifa kuendelea kuwa na amani.
Amesema Rais Dkt.Samia analiongoza vyema taifa na kuwa na upendo kwa vwananchi anaowaongoza na kumuombea afya njema na kuendelea kuliongoza taifa.
Akizungumza na waumini walioswali kwenye Msikiti huo mlinganiaji wa dini ya Kiislam kutoka mkoani Kigoma Ibrahim Mkongo amesema kuna umuhimu mkubwa wa kutoa swadaka na kuwashukuru kwa ujenzi wa Msikiti wa kisasa kupitia michango yao.
Amesema Msikiti wanaoujenga ni wa kisasa na maeneo mengine wanapaswa pia kujitoa katika kuchangia maendeleo ya uislam.
[3/31, 6:09 PM] Shomary Binda: DC CHIKOKA AZUNGUMZIA UMUHIMU WA AMANI KWENYE SWALA YA EID EL FITR
Na Shomari Binda-Musoma
MKUU wa Wilaya ÿa Musoma Juma Chikoka amezungumzia suala la umuhimu wa amani na jamii kushirikiana.
Kauli hiyo ameitoa leo machi 31,2025 kwenye Msikiti mkuu wa Ijumaa mjini Musoma baada ya kumalizika kwa swala ya Eid.
Amesema suala la amani lina umuhimu mkubwa kwenye taifa na kuwaomba waumini ya Dini ya Kiislam kuendelea kuiombea amani ya nchi wakati wote.
Chikoka amesema amani na upendo ambao umekuwepo kwenye kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhan inapaswa kuendelea katika kipindi cha miezi mingine.
Amesema katika kipindi cha mfungo unyenyekevu ulikuwa mkubwa kwa waumini na kudai yale yaliyokuwa takihubiliwa na ma Sheikh misikitini yanapaswa kuzingatiwa kwa kipindi chote.
" Tupo kwenye sherehe ya Eid baada ya kumalizika kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa waumini wa Dini ya Kiislam.
" Amani na upendo tulioishi nao kwenye kipindi hicho tunapaswa kuuendeleza kwani pasipo amani hakuna jambo lolote linaloweza fanyika",amesema.

0 Comments