Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT) imefanya Dua Maalum ya Shukrani na Kumuombea Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Uongozi wake mahili katika kipindi cha Miaka Minne ulioleta maendeleo na neema kwa Taifa la Tanzania na kuongozwa na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Ndg. Mustafa Rajab katika Msikiti wa Gaddafi Jijini Dodoma leo Tarehe 29.03.2025.
Dua hiyo Maalum imeandaliwa na Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania chini ya Mwenyekiti wake *Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC)* na Kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali Mkoa wa Dodoma. Ambayo ilienda sambamba na hafla ya Iftar kwa makundi mbalimbali wakiwemo Wajane, Watoto yatima, Madrasat na waumini wa Dini ya kiislam.
Akizungumza baada ya Dua hiyo, Mwenyekiti Chatanda ametoa wito kwa Watanzania hususani Wanawake kuendelea kumuunga Mkono Rais Samia kutokana na dhamira yake Njema ya kuwaletea Watanzania maendeleo.
"Sisi UWT tumeamua kumfanyia Dua mpendwa wetu Rais Samia kutokana na mambo makubwa aliyofanya na sisi Wanawake ni mashuhuda wakubwa" MCC Chatanda amesema.
Mwenyekiti Chatanda amesema, Mhe. Rais Samia ameimarisha Sekta ya Afya kwa kujenga na kuboresha vituo vya Afya, Zahanati na Hospitali za Wilaya na za Rufaa pamoja na uwepo wa Vifaa Tiba, na yote hayo ameyafanya katika Sekta ya Maji na Elimu"
"Hivyo UWT ina kila sababu ya kumshukuru na kumuombea Rais kwa kazi hizo nzuri. Kadharika ametoa wito wa tujitokeza Kwa wingi Kushiriki Uchaguzi Mkuu Mwezi Oktoba 2025 kumchagua na kumpa ushindi wa kishindo Mpendwa wetu Rais Samia"
0 Comments