Na Ashrack Miraji Matukio Daima App
Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Mhe. Japhari Kubecha, anamalizia mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa kufuturisha na kutoa mkono wa Eid kwa watoto wanaolelewa katika vituo vya kulelea watoto wenye mahitaji.
Akizungumza wakati wa tukio hilo, Mhe. Kubecha aliwashukuru wananchi wote waliojitokeza kushiriki iftar hii ya pamoja, akisisitiza kuwa umoja na mshikamano ni nguzo muhimu katika jamii. Aliwataka wananchi waendelee kuwa na amani, utulivu, na kushikamana wakati wote, hasa wakati wa sherehe za Sikukuu.
Pia, Mhe. Kubecha alitoa wito kwa wananchi kuendelea kumuombea Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya katika kukuza uchumi na maendeleo ya taifa. Alisema kuwa Rais Samia amekuwa mstari wa mbele katika kuleta fedha za miradi mbalimbali ambazo zinasaidia katika maendeleo ya wilaya ya Tanga, na hivyo kuchangia ustawi wa wananchi wake.
Mhe. Kubecha aliwahimiza wananchi waendelee kufanya kazi kwa bidii na kuzingatia utu katika maisha yao ya kila siku, akisema, "Kazi na utu, tunasonga mbele."
0 Comments