Header Ads Widget

UTAFITI KUHUSU CHANGAMOTO ZA USALAMA, ELIMU JUMUISHI NCHINI WAANZA





 Na Fadhili Abdallah,Kigoma


Wizara ya elimu, sayansi na teknolojia kwa kushirikiana na mpango wa shule bora wanatarajia kuendesha utafiti wa pamoja wenye lengo la kuimarisha usalama na ujumuishi wa wanafunzi katika shule za msingi nchini.


Akizungumza katika uzinduzi wa Utafiti huo katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika kwenye viwanja vya Kigano halmashauri ya mji wa Kasulu mkoani Kigoma Mratibu wa mpango wa shule bora, Morris Mkotya  alisema kuwa huo utafanyika kwenye mikoa minne ambapo kila mkoa utatoa halmashauri moja.


Morris alisema kuwa utafiti huo unakuja baada ya kuanza kutekelezwa kwa mpango wa shule bora na kugundua kukosekana kwa  mfanano katika utekelezaji wa taratibu za usalama shuleni, kiwango kisichoridhisha cha utekelezaji wa elimu jumuishi Sambamba na  ushiriki mdogo wa jamii katika kusaidia watoto mwenye mahitaji maalum.



Akizindua utafiti huo Kamishna wa elmu nchini,Dk.Lwabene Mtahaba ambaye amemwakilisha Katibu Mkuu wa wizara ya elimu,sayansi na Teknolojia Profesa Carolyne Nombo alisema kuwa  Tanzania imepiga hatua kubwa katika masuala ya elimu ikiweka  msisitizo katika elimu jumuishi na usalama wa watoto bila ubaguzi.

Dk.Lwabene alisema kuwa matokeo ya Utafiti huu yatasaidia  kufanya maboresho kwenye sera na sheria za elimu  ambazo zitasaidia kuimarisha mfumo wa elimu nchini ili kuhakikisha kuwa kila mtoto anapataa fursa sawa ya kujifunza na kufikia ndoto zake.



Akizungumza katika uzinduzi huo Afisa elimu katika sekretariet ya mkoa Kigoma, Paulina  Ndigeze alisema kuwa wamepokea fursa ya kuwa moja ya mikoa ambayo utafiti huo utafanyika na wanaamini kuwa matokeo ya utafiti huo yatakuwa na chachu kubwa katika kuhakikisha usalama na elimu ya jumuishi kwa wanafunzi wote


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI