Na Grace Mpondwe.
Katika hali isiyotarajiwa leo Machi 25, 2025 aliyekuwa mgombea wa kiti cha ubunge jimbo la Biharamulo mwaka 2020 kupitia CHADEMA amekihama chama hicho na kujiunga na CCM akipokelewa na kukabidhi kadi kwa Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Stephen Masato Wasira akiwa mkoani Kagera. Ziara hiyo ni ya kwanza kwa kiongozi huyo mkubwa wa CCM kuifanya mkoani Kagera tangu aidhinishwe na chama hicho kushika wadhifa huo mnamo 18-19 Januari, 2025.
Mwanasiasa huyo kijana amesema kuwa CCM ni chama kilichokamilika kimfumo kwa ajili ya kuiongoza nchi kuleta maendeleo huku amani ikiwa ni kipaumbele cha kudumu. Mwalimu amesema kuwa chama chake cha awali CHADEMA bado kinajisuka huku kikiteswa na zimwi la uchanga, upendeleo, utovu wa nidhamu na mikakati isiyofanya kazi.
Mwalimu alisema "CHADEMA leo wanahubiri NO HATE, NO FEAR!, kesho wanahubiri JOIN THE CHAIN!, keshokutwa wanahubiri STRONGER TOGETHER!, mtondogoo wana NO REFORM, NO ELECTION, Bangi za LEMA zikikolea kichwani anawaimbisha tena wanachama TONE TONE, mara NIMO", hakuna mkakati unaokamilika na kuleta matokeo kwa chama. Waswahili husema miruzi mingi hupoteza mbwa. Nimeamua kukihama chama hicho kwa hizo inconsistencies katika mikakati yake"
Kuhusu suala NO REFORM NO ELECTION, Mbelwa amesema CHADEMA imeibuka na mkakati huo kutokana na maandalizi hafifu ya kushiriki uchaguzi hivyo hiyo kauli inatumiwa kama kichaka cha kujifichia ili wasishiriki uchaguzi".
Mbelwa aliongeza kwa kusema kuwa "kitendo kinachopangwa na CHADEMA cha kuzuia uchaguzi usifayike ni ndoto ya mchana kwa sura moja na ni uhaini kwa sura nyingine. Mimi siwezi kuoteshwa ndoto hizo na kamwe siwezi kuendelea kufikiria kufanya uhaini wa namna hiyo kwa nchi yangu, sikuwahi kuwa mwanasiasa mwenye malengo machafu kwa nchi yangu".
Mwl. Mbelwa amesema "ni vigumu kwa chama kilichoshindwa kuweka utulivu kwenye ofisi moja ya makao makuu iliyopo Mikocheni kuleta utulivu kwenye nchi yenye kilomita za mraba 945,000 na watu wake milioni 60".
Ameongeza kuwa kutokana na mahaba waliyonayo Watanzania kwa CCM, ukipingana na CCM unajitakia taabu za maksudi pamoja na magonjwa yasiyo ya kuambukiza ikiwemo moyo kuvimba.
Amesema "Mimi Mbelwa Petro nimeona nitosheke na taabu nilizozipata kwa kuwa mwanaCHADEMA, sasa inatosha."
"Mwaka 2020 nilipogombea ubunge jimbo la Biharamulo, nilipata shida za kujitakia na baada ya uchaguzi kuisha niliambulia kuitwa Mbunge wa wananchi, nikamuuliza Mh. Mbowe, sisi wabunge wa wananchi tutakwenda kuapia wapi? Akasema, atanijibu baadae. Hajanijibu mpaka leo tarehe 25 Machi, 2025.
"Nikamuacha nikaenda kwa Kaka Lissu kwa kuwa yeye ni mwanasheria, nikamuuliza vipi Mzee sisi wabunge wa wananchi tunaapa kwa katiba ipi? Ni lini? Na wapi?".
Lissu akaniambia niwe mtulivu kwani naye yupo anatorokea Ubelgiji kutokana na hali kuwa ngumu. Nilichoka, na kupata taabu mara mbili". Aliongeza.
Mbelwa alisema "nisiseme mengi, kwa sasa nawaomba wanaCCM mnipokee, kuanzia sasa nimeacha kukunjishwa ngumi pasipo kuwa na mtu wa kupigana naye".
Kuhama kwa kada huyo linaweza kuwa pigo kwa CHADEMA jimbo la Biharamulo kwa kuwa mwanasiasa huyo alikuwa na ushawishi mkubwa hasa kwa vijana katika jimbo na mkoa mzima kwa ujumla.
SIMULIZI CHINI 👇
Licha ya kumsubiri muda mrefu ameshindwa kunioa
Jina langu ni Tina kutokea Morogoroo, mwaka 2020 nilikuwa kwenye mahusiano ambayo yalikua yanafikisha miaka 10 lakini hakuna kinachoeleweka zaidi ya manyanyaso na dharau za kutosha.
Akaoa mwanamke mwingne halafu waliposhindwana akarudi tena kwangu kuniomba msamaha, nilivvyo mjinga eti nikamsamehe, nikimuuliza lini utaenda kwetu kujitambulisha akanijibu inshallah.
Hata hivyo, kazini kwangu kulikua na mkaka ananisumbua sana lakini nampotezea eti kisa nalinda mahusiano yangu ya miaka 10 ambayo nilikuwa natarajia yatanipa ndoa lakini mambo yakawa ndivyo sivyo.
Mwisho wa siku nikachoka hali hiyo na kusafiri hadi Migori nchini Kenya ambapo nilienda kuonana na Kiwanga Doctors ambaye alinifanyia dawa za kuvuta mapenzi mapya na ndoa kupitia marriage spell.
Muda mfupi tu baada ya kuonana na Kiwanga Doctors, nikagundua huyo mwanaume kazaa na mwanamke mwingne. Nkasema dah! Inatosha nilipomuulza akanijbu ni kweli kwani kuna tatzo gani?.
Kimya kimya nikamtumia MSG yule mkaka alyekuwa ananisumbua nikamwambia sasa tunaweza kuanza maisha yetu, guess what! Nimefunga ndoa na tunaishi maisha mazuri tu hadi najuta muda wangu ambao nilipoteza kwa huyo jamaa wa kwanza.
Napoenda kutoa ushauri kwa wadada wenzangu; kuweni makini na hawa watu yaani nilianza mahusiano na ex wangu nikiwa na miaka 21 ila nimeolewa nikiwa na miaka 32 sababu ya kumsubiri yeye tu.
Mwanamke mwenzangu usikubali kupotezewa muda ukiona haeleweki kuanza upya sio dhambi, pia ukiona hakieleweki kabisa fika kwa Kiwanga Doctors ambaye anapatikana kupitia +254 116469840 au tembelea tovuti yao.
0 Comments