Header Ads Widget

BODI YA NYAMA IMEWASITISHA WANAOCHINJA NYAMA KIHOLELA KWA LENGO LA MSAADA BILA KUFATA SHERIA

 



NA CHAUSIKU SAID 

MATUKIO DAIMA.

Bodi ya nyama Mkoani Mwanza imesitisha wanaojihusisha na uchinjaji wa nyama kiholela kupitia mgongo wa utoaji wa sadaka katika maeneo mbalimbali kutokana na mazingira ya uchinjaji nyama kutokuwa rafiki na rasmi Kwa mujibu wa sheria ya Nchi na utaratibu wa utoaji sadaka, bila kufanyikia katika machinjio yaliyokaguliwa na kurasimishwa Kwa mujibu wa tasnia ya nyama .

Hayo yamebainishwa na mkaguzi na mdhibiti ubora tasnia ya Nyama Bodi ya Nyama Dr Msomi Anthony, katika kikao Cha viongozi wa dini kutoka baraza la waislamu BAKWATA na Bodi ya nyama baada ya kuwakamata watu 9 waliokuwa wakijihusisha na uchinjaji wa mifugo kiholela ili kupata Mwafaka wa namna ya kuthibiti uchinjaji holela na ugawaji wa sadaka hizo kutokana na kusambaa kwa nyama mtaani huku zikiuzwa kiholela.

Anthony ameeleza kuwa watu hao waliokuwa wakitoa sadaka walianza zoezi hilo la uchinjaji wa wanyama bila kufata misingi inayohitajika Kwa mujibu wa sheria za dini ya kiislamu na viongozi wa dini hiyo kutokuwa na taarifa juu ya uchinjaji huo.



Mkaguzi na mdhibiti ubora Tasnia ya Nyama Bodi ya Nyama Dr Msomi Anthony akilezea namna ya utaratibu wa uchingaji wa nyama ulivyofanyika kiholela.


Amefafanua kuwa uwepo wa nyama hizo mtaani huku zikizagaa na kuuzwa Kwa bei ndogo zimeweza kuathiri utaratibu wa biashara ya nyama katika maeneo mbalimbali yenye bucha na kupelekea wafanyabiashara hao kulalamikia nyama kutouzika kabsa.

"Hatutegemei baada ya hapa kuona nyama zinazagaa mtaani Kwa sababu wale wanaopewa nyama hizo ndio wanaokuja kuziuza mtaani tena, pengine zimeishahifadhiwa na kuanza kuharibika ndio zinaonekana kuanza kuuzwa na hupelekea kuathiri Afya za watu" Alisema Anthony"

Hata hivyo amewataka viongozi wa dini katika maeneo mbalimbali ambapo waumini wao wanapata misaada hiyo kuwapa elimu na kuwaelimisha juu ya sadaka hizo kuwa zinatolewa Kwa ajili ya kuwanufaisha wao na sio Kwa ajili ya kufanya biashara.

Msaidizi wa sheikh wa mkoa wamwanza Sheikh Twaha Bakari ameeleza kuwa bodi ya nyama baada ya kugundua uwepo wa watu wanaochinja nyama kiholela waliendesha zoezi la kukagua za kukagua ili kuweza kuwabaini na  kuwakamata baadhi ya wachinjaji waliokuwa wakichinja kiholela na kutoa sadaka.



Afisa mfawidhi bodi ya nyama kanda ya ziwa Nemesns Mukalaza meeleza kuwa bodi ya nyama inasimamia sheria ya nyama No 10 ya mwaka 2006 ambayo inamtaka mchungaji kuchinjia kwenye machinjio ambayo yanatambulika na yameesajiliwa na bodi nyama lakini pia nyama kusafirishwa kwenye vifaa stahiki lengo likiwa ni kulinda ubora na usalama wa bidhaa ya nyama.

        

Wakili mwandamizi wa Serikali Bodi ya nyama Tanzania Serapian Matukio ameeleza kuwa watu hao walikokuwa wanajihusisha na uchinjaji wa nyama kiholela wamekutwa na makosa 12 ambayo Kwa mujibu wa sheria ya tasinia ya nyama ya sura No421 na sheria ya ustawi wa wanyama ya mwaka 2019 na sheria ya magonjwa ya mifugo 2003 na kanuni zake za mwaka 2007 zimewakuta na makosa hayo na adhabu yake ni kifungo cha mwaka mmoja au miezi sita (6) au vyote kwa pamoja 





Baadhi ya wahubiri hao wa kiislamu waliokuwa wakichinja nyama kiholela na kutoa sadaka kinyume na taratibu na miongozo ya kuchaji nyama wamekili kufanya makosa hayo, na kuishukuru Bodi ya nyama kuwapa muongozo namna ya kufanya kazi yao kwa ufasaha na kufata sheria za nchi kwa mujibu na namna ya kugawa sadaka.

MWISHO.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI