KIJANA MWENYE ULEMAVU ALIYEUNGUA MOTO WAKATI AKIANDAA SHAMBA ASAIDIWA NA TAASISI YA FOXES
Na Matukio Daima Media
KIJANA mwenye Ulemavu Mkazi wa kijiji cha Ikanga kata ya Mdabulo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa Yusto Kalinga ambae Ulemavu wako ulitokana na kuungua moto Mwili mzima wakati akiandaa shamba kwa kuchoma nyasi amekuwa miongoni mwa Vijana wenye Ulemavu 134 wanaopatiwa Mafunzo ya ujasiriamali kupitia Taasisi ya taasisi ya Foxes Community and Wild Life Conservation na Mradi Youth Agency Mufindi (YAM).
Kijana huyo amepongeza Mradi huo wa YAM chini ya Taasisi ya Foxes Community and Wild Life Conservation na Halmashauri ya wilaya ya Mufindi kwa kumuona na kumpatia fursa hiyo ya Mafunzo .
Akizungumza Jana wakati wa Mafunzo ya Siku 12 yanayoendelea ukumbi wa Yatima Igoda Mufindi kwa Vijana hao wenye Ulemavu 134 Kijana huyo alisema kuwa Mafunzo hayo yanaelekea kumpa kipato na kuondoka na Vijana tegemezi kwa familia.
Yusto alisema kuwa malengo yake ni kuwa mfugaji mkubwa wa kuku kwa sababu kutokana na ulemavu alionao anaweza kuzifanya shughuli hizo kwa mikono yake mwenyewe na kumuingizia kipato.
Yusto ni mmoja wa walemavu 134 ambao wanapata mafunzo kupitia taasisi ya Foxes Community and Wild Life Conservation na mradi wa Youth Agency Mufindi(YAM) kutoka vijiji 16 vya kata tatu za Wilaya ya Mufindi ambazo ni kata ya Mdabulo, Luhunga na Ihanu.
"Nimechagua kufuga kuku wa kienyeji na nina hitaji kujifunza zaidi kuhusu ufgugaji ili mafunzo yatakapomalizika nitakuwa nimejua nitajikita katika kufuga mifugo gani zaidi"
Akizungumzia jinsi alivyopata ulemavu huo alisema kuwa siku moja ambayo hatoisahau katika maisha yake walikuwa wameenda kuchoma shamba na mwenzake ambaye walikuwa wakifanyakazi pamoja kwa muda mrefu walizingirwa na moto na moshi kumzidi na kujikuta kadondoka na kuungua mikono.
"Wakati tunasafisha shamba kwa kutumia moto kwa bahati mbaya moto ukatoka tulijitahidi kuuzuia lakini moshi ulituzidi na kutuzingira na kudondoka nakaungua mikono yote miwili,nimekuwa nikijiuguza kwa muda mrefu huku nikipambana kwa hali na mali ili nisiwe na ulemavu wa kudumu"
"Nawashukuru taasisi ya Foxes Community and Wild Life Conservation kwa kunisaidia kupata matibabu kutoka katika hospitali Inuka mkoani Njombe pia kufanya mazoezi ili mwisho wa siku mikono yangu iwe vizuri, nawashukuru wao kama taasisi kwa kutuwezesha kupata mafunzo na kuwekeza katika ulemavu wetu na kutufanya tuweze kujitegemee"alisema
Aliwashauri washiriki wa Mafunzo hayo ambao wanapata mafunzo katika mradi huo kusikiliza ushauri wa mkufunzi na kuwatumia katika maisha yao ya kila siku kuhakikisha yale yaliyojifunza yanaleta mafanikio katika maisha yao.
Mradi YAM Mradi ulioanza mwaka 2021 Hadi 2024 kwa kufanya kazi miaka minne kusaidia Mafunzo ya ujasiriamali na kuwawezesha Vijana wenye mazingira magumu kutoka kata tatu za Ihanu,Mdabulo na Luhunga Mradi huu umefadhiliwa na serikali ya Filands chini ya taasisi yake ya Diaconess kwa ushirikiano wa serikali ya Tanzania chini ya Halmashauri ya wilaya ya Mufindi na taasisi ya Foxes Community and Wild Life Conservation.
MWISHO.
SIMULIZI :
House girl alifanya nikaachiwa laana ya mapenzi Naitwa Hassan, kipindi nipo Chuo, likizo nikaenda kutembea kwa mjomba, sasa kutokana na maisha ya boarding, muda mrefu bila kukutanana mwanamke, nikajikuta namtolea macho house girl niliyemkuta pale.
Basi nikaanza kujenga mazoea naye, kwa vile nilikuwa mcheshi, akaingia kingi, ila akaniambia anaogopa mimba, hivyo ikabidi nikanunue condom katika duka la hapo jirani.
Siku niliyofanikiwa kulala na yule house girl, nilikuwa na papara sana, halafu sababu ya ukame nilijikuta natumia nguvu sana, uzuri yule dada alikuwa mzoefu.
Nilipomaliza, nataka kuvua condom, nakuta imepanda juu yote.
Kumbe ilipasuka bila mimi kujua, basi house girl akaanza kulia kwa wasiwasi. Nikambembeleza akanyamaza ingawa na mimi nilikuwa na wasi wasi sana kama akiwa amebeba ujauzito.
Zikapita kama siku mbili, nikashangaa pale nyumbani mjomba na shangazi wakaitisha kikao cha ghafla ambacho kilihusisha watu wote ambao tunaoishi mle ndani.
Kumbe shangazi kwenye kona ya kapeti pale sebleni aliokota kinailoni, alivyokishika kwa karibu akagundua ni kipande cha kasha la condom.
Basi kwenye kile kikao walitaka kujua ni nani aliitumia ile condom pale ndani, house girl akawekwa kati, maana yeye ndio alikuwa mwanamke pekee mkubwa, wengine ni wadogo, halafu kuna watoto wa kiume watatu wa mjomba, halafu na mimi.
House girl akawa kimya tu anasema hajui kitu, basi shangazi na mjomba wakawa wakali sana na mwisho wa siku wakasema mtu aliyefanya kitendo hicho katika nyumba yao kamwe hatakuwa na bahati katika mapenzi.
Ni kama walijua mimi ndiye nilifanya hivyo ila wakashindwa kusema hivyo wakaamua kuniadhibu kwa njia hiyo.
Huwezi kuamini kauli ile ilikuwa kama laana kwangu maana tangu siku ile kila mwanamke ambaye nilikuwa namtongoza alikuwa ananikatalia!.
Hali hiyo ilinitesa kwa miaka mingi hadi nikafikiria kurudi kwa shangazi na mjomba ili kuomba msamaha ili ndio hivyo nikawa na aibu.
Kuna jamaa yangu mmoja ikabidi nimueleze jambo hilo, naye akanishauri niende kwa Kiwanga Doctors kwa msaada zaidi.
Hivyo nilisafiri hadi Migori, Kenya kwa Kiwanga Doctors ambaye ni mtaalamu wa tiba asilia na kumueleza shida yangu hiyo.
Mara moja aliamua kunifanyia love spell na marriage spell ili kurejesha tena bahati yangu katika mapenzi.
Na kweli baada ya muda hali ile ikaandoka na sasa nina mahusiano ambayo yapo imara sana. Ikiwa nawe unahitaji huduma hiyo basi chukua hatua ya kuwasiliana na Kiwanga Doctors kwa namba +254 116 469840 au tembelea tovuti yao.
0 Comments