Header Ads Widget

KAIMU KAMISHNA WA UHIFADHI TAWA AFUNGUA KIKAO CHA MAANDALIZI YA BAJETI YA TAWA

 


Na. Joyce Ndunguru, Arusha.

Kaimu Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Mlage Kabange leo 11 Machi, 2025 amefungua rasmi kikao kazi cha maandalizi ya bajeti ya TAWA kwa Mwaka wa fedha 2025/2026 kilichofanyika katika ukumbi wa Ngorongoro jijini Arusha.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao hicho, Kamishna Kabange amesema maksio ya bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026 yanapaswa kujielekeza katika vipaumbele vya Mamlaka ambavyo ni pamoja na ulinzi wa rasilimali za wanyamapori na malikale, utatuzi wa migogoro ya mipaka na udhibiti wa wanyamapori wakali na waharibifu pamoja, kuimarisha utalii na kuongeza mapato pamoja pamoja na kuimarisha mazingira ya utendaji kazi kwa watumishi.

"Katika ulinzi wa rasilimali ya wanyamapori nawaelekeza kuendelea kuimarisha ulinzi wa maeneo yetu ya hifadhi ikiwa ni pamoja na kuendelea kusimamia kikamilifu masuala ya doria" amesema Kamishna Kabange.

Kadhalika, Kamishna Kabange amewaelekeza Makamanda wa Kanda kuweka mikakati madhubuti ya kuongeza idadi ya watalii pamoja na mapato.

Pamoja na hilo, Makamanda wa Kanda wametakiwa kuhakikisha watumishi wanazingatia sheria, kanuni zilizopo sambamba na taratibu za kijeshi ili kudumisha nidhamu na kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu.

Pia ameelekeza utunzaji wa vitendea kazi yakiwemo magari ya doria na miundombinu mbalimbali iliyojengwa katika maeneo wanayosimamia.












Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI