SELIKALI ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia S. Hassan imefanya jitihada kubwa katika sekta ya elimu, ambapo mwaka huu wa fedha zimetengwa bilioni 16.
Katika muktadha huo, Mbunge wa Dodoma Mjini, Antony Mavunde, amegawa komputa na printa kwa shule zote za sekondari katika jimbo lake.
Tukio hilo lilifanyika jijini Dodoma katika Shule ya Sekondari Viwandani.
"Nataka Dodoma kuwa kinara katika matumizi ya teknolojia katika ufundishaji, " Amesema Mavunde.
Aidha Kompyuta alizogawa zimewekewa mitihani yote kuanzia mwaka 1988 hadi 2024 kwa kidato cha II, IV, VI, pamoja na vitabu vya ziada na kiada, simulation za masomo ya sayansi, video tutorials, na notes za masomo.
Kwa upande wke Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Alhaji Jabir Shekimweri, amepongeza Mavunde kwa juhudi zake katika kuboresha sekta ya elimu na mipango ya kuziunganisha shule zote za Dodoma na Internet.
Naye Diwani wa Kata ya Viwandani, Jafary Manyemba, alishukuru Mbunge kwa ukarabati wa maabara na utoaji wa vifaa katika shule mbalimbali, akiwataka wanafunzi kutumia fursa hii ili kuongeza maarifa na kufanya vizuri kwenye mitihani yao.
0 Comments