Header Ads Widget

SHEIKH KWEZI AWAOMBA WATANZANIA KUENDELEA KUMUOMBEA RAIS DKT.SAMIA

 


Na Shomari Binda-Simiyu

SHEIKH Mkuu wa Mkoa wa Simiyu isaa Kwezi amewaomba Watanzania kuendelea kumuombea dua Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ili awe na afya njema na kuendelea kuwahudumia.


Hayo ameyasema alipokuwa akizjngumza na Matukio Daima Mara baada ya kumalizika kwa ziara yake mkoani humo.


Amesema Rais Dkt.Samia amekuwa akiangaika huku na kule katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma mbalimbali kwemye maeneo yao.


Sheikh zkwezi amesema miradi ambayo ameizindua mkoani Simiyu Inakwenda kuwasaidia wananchi kiuchumi ikiwa ni pamoja na elimu ya mafunzo kwa wanafunzi.


Amesema kuombewa dua ya kuwa na afya njema kwake kutaendelea kumpa afya na nguvu kuendelea kuwatumikia wananchi.


" Ziara ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan imekuwa na manufaa makubwakoani Si

Minutes kwani tumeona miradi mbalimbali ikifunguliwa.


" Jambo jema ni kuendelea kumuombea dua awe na afya njema na kuendelea kuwatumikia na kuwahudumia wananchi na kuleta maendeleo",amesema.


Shekh Kwezi amesema miradi yote iliyofunguliwa mkoani Simiyu wasamizi wake waisimami vizuri ili lengo na makusudio yake yaweze kutekelezwa.


Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan amehitimisha ziara yake ya siku 4 mkoani Simiyu kuzindua miradi mbalimbali kwenye sekta za afya,elimu,kiliml,mifugo na uwekezaji na hii leo ataanza ziara mkoani Mwanza na kuzindua daraja la kimkakati la Kigogo"Busisi maarufu daraja la Magufuli.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI