Header Ads Widget

MAKALA AWAPA KONGOLE TANROADS SIMIYU.

KATIBU wa Halmashauri Kuu (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Itikadi, Uenezi, Siasa na Mafunzo, CPA Amos Makala, akiongea na Meneja wa TANROADS Mkoa wa Simiyu, Mhandisi Boniphace Mkumbo (wa kwanza kulia).


Na COSTANTINE MATHIAS, Simiyu.


KATIBU wa Halmashauri Kuu (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Itikadi, Uenezi, Siasa na Mafunzo, CPA Amos Makala amewasili Mkoani Simiyu kwa ajili ya kushiriki Maadhimisho ya Miaka minne ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan huku akiwapongeza Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Simiyu kwa kufanya kazi vizuri.


Ameyasema hayo leo March 22, 2025, ambapo amesema Wakala huo umetekeleza miradi mbalimbali ya Barabara katika Mkoa huo na kufungua fursa za kiuchumi, usafiri ma usafirishaji.


Akimtolea Mfano Meneja wa Wakala huo Mkoa wa Simiyu, Mhandisi Mkumbo ambaye amefanya kazi vizuri akiwa Mkoa wa Mwanza na kumtaka aendelee kuchapa kazi katika kuwatumikia Watanzania kwenye sekta ya Barabara.

"Namfahamu, Mhandisi Mkumbo, tuliwahi kufanya nae kazi...akiwa Mwanza amefanya kazi kubwa, naomba na hapa endelea kuchapa kazi ili kuwatumikia wananchi" amesema Makala.


Awali akimkaribisha Makala katiba banda na TANROADS, Meneja Mkumbo amesema miradi mingi ya Barabara katika Mkoa wa Simiyu imetekelezwa na kufungua fursa za usafiri na usafirishaji.

 

"Tumepewa shilingi Bil. 8 kwa ajili ya kujenga Daraja la Mto Itembe, tumejenga Barabara za mizunguko (roundabout) mjini Bariadi na Lamadi, Bypass Maswa na maeneo mengine ujenzi unaendelea" amesema Mhandisi Mkumbo.


Mwisho.




Wafanyakazi wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Simiyu wakiwa kwenye Banda wakati wa maadhimisho ya Miaka 4 ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.








Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI