KATIBU Mwenezi wa CCM, CPA Amos Makala akiongoza na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Kenani Kihongosi.
Na COSTANTINE MATHIAS, Simiyu.
KATIBU wa Halmashauri Kuu (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Itikadi, Uenezi, Siasa na Mafunzo, CPA Amos Makala amewasili Mkoani Simiyu kwa ajili ya kushiriki Maadhimisho ya Miaka minne ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.
CPA Makala, amepokelewa na wenyeji wake akiwemo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Shemsa Mohammed pamoja na Mkuu wa Mkoa huo Kenani Kihongosi pamoja na viongozi wengine kutoka wilaya za Mkoa huo.
Mara baada ya kupokelea ametembelea Mabanda mbalimbali ya Taasisi za Serikali na sekta binafsi ambazo zilielezea Mafanikio ya Miaka minne ya Serikali ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.
0 Comments