Na Matukio Daima Media
Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa kupitia Wilaya ya Iringa Vijijini, Festo Kiswaga, amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mgombea urais wa CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, anajiuza kwa kazi kubwa za maendeleo anazozifanya nchini.
Kiswaga aliyasema haya alipokuwa akizungumza na Matukio Daima TV Jana kuwa utendaji wa Rais Samia unajidhihirisha wazi kwa kila Mtanzania, hata kwa wapinzani wa kisiasa, akiwemo Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Tundu Lissu, ambaye naye anatambua kazi zinazofanywa na serikali ya awamu ya sita.
Kiswaga alibainisha baadhi ya miradi mikubwa ya maendeleo ambayo imekuwa na manufaa kwa wananchi wa Iringa na Tanzania kwa ujumla. Miradi hii ni pamoja na
Kuwa Kwa upande wa Sekta ya Miundombinu kuwa Serikali imeendelea na ujenzi wa barabara za lami, madaraja na njia za reli, ikiwa ni pamoja na mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) na barabara za vijijini zinazorahisisha usafiri na biashara.
Kiswaga alisema katika Afya kumekuwepo na Uboreshaji wa huduma za afya kwa kujenga na kukarabati hospitali, vituo vya afya, na zahanati umewezesha wananchi kupata huduma bora karibu na makazi yao.
Kuwa Serikali pia imeendelea kusambaza vifaa tiba muhimu vya Elimu .
"Serikali imetekeleza sera ya elimu bila malipo kwa shule za msingi na sekondari, huku ikiwekeza kwenye ujenzi wa madarasa, mabweni, na vyuo vya ufundi ili kuboresha mazingira ya kujifunzia
Alisema kuwa Rais Samia ameendelea kusimamia utekelezaji wa miradi ya kilimo na upatikanaji wa maji safi na salama, hasa vijijini, ili kuboresha maisha ya wakulima na kuongeza uzalishaji wa chakula na mazao ya biashara.
Kiswaga alisema Kuhusu mikutano ya kampeni ya Tundu Lissu mkoani Iringa, hususan kaulimbiu yake ya No Reform, No Election, Kiswaga alisema kuwa kampeni hiyo haina mashiko kwa wananchi wa Iringa, kwani tayari wanatambua mafanikio ya Rais Samia na serikali yake.
Alisema kuwa licha ya Lissu kuendelea kusisitiza haja ya marekebisho ya mfumo wa uchaguzi, wananchi wa Iringa wanaona maendeleo halisi yaliyofanywa na serikali ya CCM, na hivyo hawawezi kushawishika kuunga mkono harakati ambazo hazina msingi kwao.
Festo Kiswaga, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Monduli, aliwataka wananchi wa Iringa na Tanzania kwa ujumla kuendelea kumuunga mkono Rais Samia ili aweze kuendeleza miradi mikubwa ya maendeleo aliyoianzisha.
Alisema kuwa zawadi pekee ambayo Watanzania wanaweza kumpa Rais Samia ni kumpigia kura kwa wingi katika uchaguzi mkuu ujao ili aweze kuendelea kuwatumikia kwa ufanisi zaidi.
Hata hivyo alisema kuwa hata wapinzani wa kisiasa, ambao mara nyingi wamekuwa wakikosoa serikali, wanakiri kuwa maendeleo yaliyofanywa na Rais Samia ni ya kiwango cha juu na yameleta manufaa kwa wananchi wa kada zote, bila kujali itikadi zao za kisiasa.
"Kazi nzuri za Rais Wetu kipenzi Dkt Samia Suluhu Hassan inadhihirisha namna utendaji wake unavyotambuliwa na viongozi wa chama tawala na hata baadhi ya wapinzani "
Kuwa akiwa kiongozi wa serikali na mjumbe wa Mkutano mkuu wa CCM Taifa anasisitiza kuwa siasa za maendeleo ndizo zinazowapa wananchi sababu ya kumwamini Rais Samia, badala ya siasa za kupinga kila jambo.
0 Comments