Header Ads Widget

AUSWA WAFANIKISHA UPATIKANAJI WA MAJISAFI ASILIMIA 99

 


Na Hamida Ramadhan Matukio Daima App Dodoma

MKURUNGEZI  Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jiji la Arusha (AUWSA), Mhandisi Justine G. Rujomba amesema eneo la Jiji la Arusha kwa kupitia Mradi mkubwa, AUWSA imefanikisha upatikanaji wa majisafi kwa asilimia 99.

Ameyasema hayo wakati waandishi wa habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa ofisi hiyo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita, leo Machi 14, 2025, katika Ofisi za Idara ya Habari - MAELEZO, jijini Dodoma.

Amesema Uboreshaji wa Huduma ya MajitakaAUWSA imepanua mtandao wa kukusanya majitaka kutoka asilimia 8.03 (2020/21) hadi asilimia 39.5 mwaka 2024/25. 

Aidha amesema mafanikio Katika Upatikanaji wa Majisafi

Katika mwaka wa fedha 2024/25,  umeongezeka kwa kiwango kikubwa ambapo AUWSA imeendelea kupanua mtandao wa usambazaji majisafi ili kutekeleza dhamira ya Serikali ya kuhakikisha wakazi wa mijini wanapata huduma ya majisafi na salama kwa asilimia 95 ifikapo 2025. 

Aidha, ili kuwahudumia wananchi ambao hawajafikiwa na mtandao wa majitaka, AUWSA imenunua magari manne ya kunyonya majitaka (Cesspit Emptier Trucks), yenye uwezo wa kubeba lita 5,000 na 10,000.

"Majitaka yanayokusanywa kutoka kwa wateja zaidi ya 10,930 yanatibiwa katika mabwawa ya kutibu majitaka yaliyopo Terrat (Themi Holding Ground) ambapo majitaka hayo yaliyotibiwa yanawanufaisha wananchi walipo kusini mwa mabwawa hayo kwa kutumia maji hayo yaliyotibiwa kwa shughuli za kiuchumi hususani kilimo cha umwagiliaji, " Amesema

Amesema Masaa ya upatikanaji wa huduma ya maji yameongezeka kutoka saa 16 (2020/21) hadi saa 22 mwaka 2024/25. 

Aidha, idadi ya wateja waliounganishwa na huduma za maji imeongezeka kutoka 71,183 (Juni 2021) hadi 134,000 kwa sasa.

Amesema utekelezaji wa Miradi ya Maji

Kupitia ufadhili wa Serikali ya Tanzania Pamoja na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), AUWSA imekamilisha mradi mkubwa wa maji kwa lengo la kuboresha hali ya upatikanaji wa majisafi na kuboresha huduma ya uondoaji wa majitaka katika jiji la Arusha ili kuboresha afya na hali ya maisha ya wakazi wa Jiji kwa ujumla wake.

Amesema kazi zilizofanyika ni pamoja Uchimbaji wa visima virefu, ujenzi wa mabwawa ya kutibu majitaka, Ujenzi wa mtambo wa kutibu majisafi katika chanzo cha mto - Midawe,

Upanuzi wa mtandao wa majitaka pembezoni mwa Mji, Ujenzi wa vyoo vya mfano katika shule na masoko, Ujenzi wa Ofisi za Kanda na Ofisi Kuu kwa lengo la kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi pamoja na Upanuzi wa mtandao wa majisafi.

Amesema Miradi mingine inayoendelea kutekelezwa na AUWSA ni Mradi wa Majisafi Mlangarini;

Mradi huu unagharimu TZS bilioni 3.7 na utahudumia wakazi 9,100 katika kata za Moivaro, Moshono na Mlangarini. Mradi umekamilika na sasa wananchi wameanza kuunganishiwa huduma ya maji.. 

Amesema Mradi wa uondoaji wa majitaka A – Z

Mradi huu unagharimu TZS bilioni 2.5 na utahudumia wakazi zaidi ya 1,200 katika kata ya Olmoti, umefikia asilimia 60 ya utekelezaji.

Amesema Mradi wa Majisafi Imbaseni

Mradi huu unagharimu TZS bilioni 1.9 na utahudumia wakazi wapatao 19,578 katika vijiji vya Ngongongare, Kiwawa na Imbaseni na kwa sasa utekelezaji wake utafikia asilimia 55.

Ameeleza Mradi wa Majisafi Enguik – Monduli

Mradi huu unagharimu TZS bilioni 2.9 utahudumia wakazi wapatao 15,200 katika kata ya Monduli juu vijiji vya Emairete, Enguiki na Elwai na kwa sasa umefikia asilimia 67 ya utekelezaji.

Amesema,Mradi wa Majisafi Vijiji Nane – Ngorongoro

Mradi huu unagharimu TZS bilioni 6.1 na utahudumia wakazi wapatao 33,969 katika vijiji vya Ng’arwa, Olorien, Magaiduru, Mageri, Mugongo, Tinaga, Yasi na Mdito na kwa sasa utekelezaji wake umefikia asilimia 52.

Ameeleza,Mradi wa Vijiji Saba – Arumeru

Mradi huu unagharimu TZS bilioni 8.6 na utahudumia wakazi wapatao 35,079 katika vijiji vya Maweni, Karangai, Msitu wa Mbogo, Shambarai Burka, Migungani, Valeska na Patanumbe, na uko katika hatua za awali za utekelezaji.

Mradi wa Majisafi Oldonyosambu

Mradi huo unagharimu TZS bilioni 6.3 na utahudumia wakazi wapatao 29,449 katika vijiji vya Oldonyosambu, Lemanda, Lemong’o, Oldonyowasi na Lesinoni na kwa sasa utekelezaji wake umefikia asilimia 50.











Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI