Header Ads Widget

ANDENGENYE ARIDHISHWA NA UTENDAJI WA TASAC

 

Mkuu wa mkoa Kigoma Thobias Andengenye.



Na Fadhili Abdallah, Kigoma 


MKUU wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye ameupongeza Uongozi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) kwa  kusimamia shughuli za usalama wa usafirishaji kwa ufanisi jambo linaloendelea kuimarisha usalama na ukuaji wa uchumi wa nchi mkoani humo.


Andengenye ametoa pongezi hizo alipofanya mazungumzo na Afisa Mfawidhi wa TASAC , Adam Mamilo aliyefika ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa lengo la kujitambulisha mara baada  kuwasili katika kituo chake kipya cha kazi Mkoani hapa. 


Mkuu huyo wa mkoa amesema kuwa TASAC  inapaswa kuongeza nguvu katika kusimamia huduma za usalama wa usafirishaji majini hususani katika bandari za Kigoma kutokana kasi ya serikali kufanya maboresho makubwa ya miundombinu kwenye bandari za mkoa huo hali inayovutia wafanyabiashara kutoka nchi za ukanda wa maziwa makuu kutumia bandari hiyo. 


Kwa upande wake Katibu Tawala Mk wa Kigoma Hassan Rugwa amesema  fursa za kiuchumi zitokanazo na Ziwa Tanganyika zimechangia ongezeko kubwa la vyombo vya uchukuzi visivyo rasmi vinavyochangia kuhatarisha usalama wa wananchi wanaovitumia, hivyo TASAC wanalo jukumu kubwa la kusimamia shughuli za usalama usafirishaji ziwani.


Pamoja na hilo alisema kuwa serikali imeamua kuwekeza katika uboreshaji miundombinu ya uchukuzi ikiwemo ukarabati wa Meli ya Mt. Sangara, Mv Liemba pamoja na Mv. Mwongozo ambapo ameitaka TASAC kusimamia na kuhakikisha ukarabati wa meli hizo unakamilika kwa wakati ili tuweze kukabiliana na mahitaji makubwa ya usafirishaji wa abiria na mizigi.



Akizungumza mbele ya Mkuu wa mkoa Afisa Mfawidhi wa TASAC Kigoma, Adam Mamilo ameahidi kushirikiana na viongozi wa Serikali ya Mkoa kwa ajili ya kupokea ushauri utakaolenga kuhakikisha miradi mbalimbali inayotekelezwa kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi wa Bandari inakamilika kwa wakati.


Mwisho.

Viongozi wa TASAC (kulia) wakitoa taarifa kwa Mkuu wa mkoa Kigoma Thobias Andengenye (aliyekaa kushoto).





Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI