Header Ads Widget

BRAC YASHEREHEKEA MIAKA 53 KWA KUTOA MSAADA KWA WANAFUNZI YATIMA

 

Wananfunzi wa Shule ya Sekondari Bethasadia wakipokea msaada wa vifaa maalumu na rasilimali elimu kutoka Shiroka la BRAC Tanzania
Mkurugenzi wa BRAC Tanzania, Joydeep Sinha Roy akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Bethasaida walipotembelea na kutoa msaada wa vifaa muhimu na rasilimaliza elimu kwa wasichana hao, hilo limefanyika wakati wa kuadhimisha miaka 53 toka kuanzishwa kwa Shirika hilo.

Na Elizabeth Zaya

TAASISI isiyo ya kiserikali BRAC Tanzania imesherehekea  mwaka wake wa 53 tangu kuanzishwa kwake kwa kutoa vifaa muhimu na rasilimali za elimu kwa ajili ya kusaidia uwezeshaji wa wasichana katika shule ya Sekondari  Bethsadia ya wasichana ya watoto yatima.

Katika kurudisha kwenye jamii katika kusherehekea miaka hiyo,  wafanyakazi wa BRAC wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wake, Joydeep Roy, wametoa msaada wa vifaa mbalimbali vya elimu katika shule hiyo iliyopo Mbezi Mpiji Magohe mkoani Dar es Salaam.


 


Joydeep, akizungumza na wanafunzi hao baada ya kufika Shule katika shule hiyo, amesema kujitolea kwao kutoa misaada ya kurejesha kwa jamii, ni katika kuonesha namna wanavyojikita kwenye masuala ya kijamii hususani uwezeshaji watoto wa kike.


Kadhalika, amesema kufanya hivyo ni kuiunga mkono serikali pamoja na watunga sera katika kusaidia jamii kupunguza umasikini.


"Lengo ni kuendelea kushirikiana na serikali, watunga sera, na mashirika ya kimataifa kwa ajili ya kupunguza umaskini ambapo kupitia shirika letu tunatoa mchango wetu katika huduma za kifedha, makuzi, malezi na maendeleo ya awali ya watoto wadogo, uwezeshaji wa vijana, elimu, kilimo, na programu ya uondoaji umasikini uliokithiri,"amesema Joydeep.


Amesema taasisi hiyo imekusudia kukuza umoja na ushirikiano wa ndani kupitia mijadala.


“Mikutano hii itatoa jukwaa kwa wafanyakazi kushiriki mawazo kuhusu changamoto, uvumbuzi, mambo chanya na halisi ya kazi wanayokutana pamoja na washiriki kutoa ushuhuda kutoka kwa washiriki wa programu mbalimbali na wananchi kuhusu mambo mbalimbali yanayoendeshwa na taasisi yetu,”amesema Joydeep.

Amesema kupitia programu mbalimbali za kutoa huduma za kurejesha kwa jamii, tayari wamewafikia watu milioni 1.4.

Mwenyekiti na mwanzilishi wa Shule ya Sekondari  Bethsadia , Raymond Machary amewashukuru BRAC Tanzania kwa kuwakumbuka mabinti hao ambapo wengi wao bado wanahitaji msaada huo kwa sababu shule hiyo inachukua wanafunzi wenye uhitaji ambao wengi wao hawana wazazi.

“Yapo mashirika na taasisi ambazo zinaweza kujitolea kwa ajili ya wanafunzi hawa, kikubwa ni kuwa na moyo wa kujitolea kama walivyofanya shirika la BRAC, na mimi kama kiongozi mkuu wa shule hii ya wasichana nakaribisha makundi yote,”amesema Mashary.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI