Header Ads Widget

TUME YA HAKI ZA BIBADAMU NA UTAWALA BORA KUKUTANA NA MAKUNDI MBALI MBALI MKOA WA IRINGA

 

Kamishina wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora Dkt Thomas Masanja akizungumza na wanahabari Iringa ,kulia ni mwanasheria wa mkoa wa Iringa 

NA BERDINA MAJINGE MATUKIO DAIMA MEDIA ,IRINGA 

Tume ya haki za binadamu na utawala bora nchini imesema kuwa inatarajia kutoa elimu katika maeneo ambayo wananchi wanazuiliwa kufika ili kuwasaidia watu walioko katika mazingira hayo kujua haki zao za msingi.


Elimu hiyo itatolewa katika magereza, kituo cha Polisi cha kati wakiangalia viwango vya uzingatiaji wa haki za binadamu katika maeneo hayo na ufuatiliaji wake.

Akizungumza na wanahabari mkoani Iringa leo   Feb,18,2025  Kamishina wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora Dkt Thomas Masanja alisema kuwa wanatarajia kutoa elimu hiyo maeneo mbalimbali katika mkoa huo kwa siku 20.

Dkt Masanja alisema kuwa elimu hiyo itatolewa kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu, wanafunzi wa shule za sekondari, watendaji wa mitaa na vijiji, magereza na kituo cha polisi cha kati mkoani Iringa.


"Tuko Mkoani hapa kuendeleza haki za binadamu na utawala bora ikiwa ni pamoja na kutoa elimu na kufanya tafiti mbalimbali juu ya masuala ya haki za binadamu na kuishauri serikali juu ya masuala yanayokiukwa kwa wananchi"

Mwenyekiti wa Chama Cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa Frank Leonard akitoa neno la ukaribisho 

Alisema kuwa tume inaangalia na kuwafikia watu wenye ulemavu wa ngozi kwa kufanya mikutano ya hadhara kupitia watendaji wavijiji.


"Mwananchi anapokuwa gerezani anakuwa amenyang'anywa uhuru lakini haki zake zingine zote anabaki nazo ikiongozwa na haki ya utu wa mtu ambayo kila mtu anazaliwa nayo, pia haki zingine ni kupata matibabu pamoja na chakula"


Dkt Masanja alieleza kuwa kupitia watendaji wa vijiji na wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu na shule za sekondali watafanikiwa kuwafikia wananchi wengi kupata elimu ya haki za binadamu na utawala bora.


Akizungumzia suala la wananchi kukamatwa siku ambazo si kazi na kunyimwa dhamana siku hizo Dkt Masanja alisema kuwa sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai ni mtu atakamatwa na kuwekwa kizuizini mpaka pale upelelezi utakapo kuwa umekamilika lakini makosa mengine yanaelekeza baada ya uchunguzi na kujiridhisha kuwa hana hatia mtuhumiwa ataachiwa au kupewa dhamana.


Dkt Masanja alisema kuwa suala la wananchi kupotea au kuwa katika mazingira ambayo hayajulikani alisema kuwa tayari tume imetoa tamko  na kusema kuwa wangefanya ufatiliaji kwa watu wanaodaiwa kupotea na walifanyakazi hiyo November 2024.

MWISHO

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI