Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Tabia za wazazi Wengi kushindwa kuwalea watoto katika malezi yenye maadili mema imetajwa kuendelea kuliingiza Taifa kwenye misukosuko na mmomonyoko wa maadili kwa watoto wanaoweza Kukengeuka na kujiingiza kwenye makundi hatarishi.
Tabia hizo zinatajwa kuwafanya watoto Wengi kuwa wezi,majambazi na Wengine kujiingiza kwenye vitendo vya ushoga na usagaji ambapo Katibu wa Elimu wa Jumuiya ya wazazi wilaya ya Ludewa Bazil Makungu wakati wa Maadhimisho ya miaka 48 ya kuzaliwa kwa Chama Cha mapinduzi amesema wazazi wanapaswa kuwa makini.
Viongozi wa CCM chini ya Jumuiya ya wazazi mkoa wa Njombe baada ya kushiriki zoezi la kupanda miti kazunguka eneo la shule ya Sekondari Mavanga wilayani Ludewa Wametoa mada mbalimbali kwa wanafunzi hao huku Jolam Hongoli mjumbe wa kamati ya utekelezaji Jumuiya ya wazazi amewasisitiza wanafunzi kuzingatia Nidhamu kwani ndiyo itawasaidia kufanya vizuri katika masomo yao.
Kwa upande wake Afande Neema Lutufyo kaimu mkuu wa Dawati la Jinsia wilaya ya Ludewa na Rabson Mahenge Mjumbe Baraza la wazazi CCM Taifa mkoa wa Njombe wamesema vitendo vya ukatili,Ushoga na usagaji vinatokana na Kukengeuka kimaadili Tangu wadogo jambo ambalo elimu inatakiwa kutolewa kwa kiwango kikubwa.
Hata hivyo Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi CCM mkoa wa Njombe Gelard Mpogolo pamoja na katibu wake Emmanuel Ngulugulu wamesema Kazi kubwa ya Jumuiya ya wazazi ni kuelekeza maadili mema kwa jamii na ndio sababu ya kufika katika shule hiyo na kuzungumza nao.
Samuel Haule na Faraja Mgina ni Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mavanga ambao wanaahidi kuendelea kuzingatia masomo kama walivyofanya watangulizi wao kidato Cha nne kwa kuwa shule ya kwanza kwa wilaya ya Ludewa huku Joseph Mapunda mkuu wa shule hiyo akishukuru kwa elimu iliyotolewa na zawadi mbalimbali.
Shule ya Sekondari Mavanga Ina Jumla ya wanafunzi 528.
0 Comments