Header Ads Widget

CHANGAMOTO YA UKOSEFU WA MITAJI KWA VIJANA MOROGORO

 

Na Lilian Kasenene,Morogoro

Matukio DaimaApp 

UKOSEFU wa mitaji ya kuendeleza biashara kwa vijana wajasiliamali wadogo katika Halmashauri ya Wilaya Morogoro ni miongoni mwa changamoto zinazowakabili vijana hao kufikia malengo yao.

Akisoma risala kwa niaba ya vijana wenzake,Easter Mtwale amebainisha hayo kwenye mdahalo wa mapitio ya kisera zenye kuweka mazingira endelevu kwa vijana ili kuweza kujitegemea. 

Vijana hao wamebainisha kuwa licha ya kupatiwa mafunzo na kuwezeshwa vifaa vya kusindikaji wa mazao ya viungo kutoka shirika lisilo la kiserikali la Mviwamoro waiomba serikali kuweka mazingira mazuri ya upatikaji wa ardhi itakawofanya kupanua shughuli zao na kuondokana na utegemezi.

"Pamoja na jitihada hizi tunakumbana na changamoto mbalimbali zinazokwamisha ukuaji wa biashara zetu ambazo ni ukosefu wa ardhi ya kufanyia shughuli kwa uhakika na endelevu,"walisema

Aidha,vijana hao wamebainisha kwa wanahitaji ushauri wa kibiashara kutoka kwa maafisa biashara wa serikali.

Afisa wa Serikali,ofisi ya mkuu wa mkoa wa Morogoro Peter Gama  kwa upande wake alisema serikali imeandaa mazingira mazuri katika kuhakikisha Kila halmashauri inatenga asilimia 10 ya mapato yake ndani kwa ajili ya kutoa mikopo isiyo na riba kwa makundi ya vijana,wanawake na walemavu ili waweze kujikwamua kiuchumi.


Gama alisema kuwa katika asilimia 10 hizo,asilimia ni 4 kwa ajili ya vijana,asilimia 4 kwa wanawake na asilimia 2 kwa ajili ya watu wenye ulemavu.


Pia,aliahidi kuwa changamoto zilizoanishwa na vijana kwenye risala yao zinazohusu sera zitashughulikiwa katika mamlaka husika hatua kwa hatua ikiwa ni dhamira ya serikali kuzipatia ufumbuzi changamoto za kimfumo zinazowakabili wananchi.


Aliwaasa vijana kukitambua na kuchangamkia fursa zinapojitokeza badala ya kujifungia bila ya kujitangaza.

Sanjari na hilo,amelipa kongole shirika la Mviwamoro kwa uwezeshaji kwa vijana kwa kupatiwa mafunzo na  vifaa vya ushindaji wa mazao ya viungo ambavyo vinazalishwa na wakulima katika maeneo ya vijijini 

Kwa upande wake, Joseph Sengasenga ambaye ni mratibu wa shirika lisilo la kiserikali la Mviwamoro amesema wamefanikiwa kuwaunganisha vijana katik vikundi 18 kutoka vijiji vya kingole, mtamba, mkombozi, Tawa, Nige, kibangile kwa lengo la kutengeneza ajira na kipato kwa vijana kupitia mnyororo wa thamani.

Sengasenga asema Taasisi yake inawatengenezea vijana Fursa kwa kuwaunganisha na wadau wengine ikiwemo sido ambapo pamoja na shughuli nyingine wanazofanya pia wanatoa mikopo kwa mtu mmoja mmoja 

Alisema kuwa licha ya kuwa suala la mkopo ni la mtu binafsi lakini vijana wanapaswa kujitambua na kujiongeza katika kuendeleza biashara zao kwenye hoteli na miji mikubwa,Dodoma,Dar es Salaam badala ya kubaki maeneo ya vijijini.

"Vijana waliopata fursa katika halmashauri ya morogoro vijijini tumewawezesha kwa kuwapa vifaa vya kusindika bidhaa za viungo kama iriki,karafuu,matunda kama mafenisi  ni wajibu wao sasa kutafuta soko ili kujiongezea kipato," alisema.

Katika mdahalo huo umewakutanisha wataalamu mbalimbali kutoka Halmashauri, viongozi wa serikali pamoja na madiwani.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI