Afisa Kilimo Wizara ya kilimo idara ya maendeleo ya mazao Alphonce Mwiru wa pili kushoto mwenye kofia akiwa na meneja wa Iringa Co . Operative union Tumain Lupola wa kwanza kulia Leo baada ya kutembelea Chama hicho picha na Matukio Daima media
NA MATUKIO DAIMA MEDIA,IRINGA
WAKULIMA wa zao la Tumbaku Mkoani Iringa wametakiwa kujiungana na vyama ushirika wa Kilimo na Masoko (AMCOS), ili waweze kunufaika na mbole ya ruzuku zinazo tolewa na Serikali.
Wito huo umetolewa leo na Afisa Kilimo Wizara ya Kilimo idara ya maendelea ya mazao Alphonce Mwiru aliyefanya ziara na timu yake kukagua maendeleo ya mbolea hiyo .
Alisema fulsa nyingi hutokea pindi mkulima ananapo jiunga na vyama vya Ushirika ni Moja ya nguzo Yao kwani wapo mkoani Iringa kwa ajili ya kufuatilia pembejeo za Kilimo hasa kwenye mbolea za ruzuku za zao la tumbaku.
"Tunaenda mikoa mbalimbali kule ambapo mbolea imesambazwa na wanapolima tumbaku tumeanza Morogoro kwenye chama cha wakulima wa tumbaku ambacho kimeunganisha umoja wa vyama vya tumbaku nchini."alisema
Afisa Kilimo Wizara ya Kilimo idara ya Maendeleo ya mazao Aphonce Mwiru (Mwemyekofia pama) akiwa na wakulima wa tumbako wanachama wa Chama Cha Ushirika Cha wakulima Iringa (Iringa Farmers Co.Operative Union IFCU 1993 LTD) Leo baada ya kutembelea wakulima hao kuona Matokeo ya mbolea ya Ruzuku kwa zao la Tumbaku
Kuwa chama cha wakulima Iringa ( Iringa Farmers CO .Operative union -IFCU 1993 LTD) kipo vizuri kwa sababu kinashughulika na mbolea za ruzuku nje na tumbaku lakini kuna mbolea zingine za mazao mengine.
"Tumeshauri kwa kuwa chama cha Iringa
Iringa Farmers Co-operative union kina chama kimoja cha tumbaku na ndicho kimejiunga muda sio mrefu.
"Tumeshauri kwa kuwa chama cha Iringa Farmers Co.Operative Union kina chama kimoja cha tumbaku na ndicho kimejiunga muda sio mrefu,
tumeshauri vyama vingine viweze kujiunga lakini pia viweze kujiunga kwenye umoja wa TCGAE ili waweze kusaidiwa zaidi
kwa sababu wanachama kimoja"
Mwiru alisema kuwa wanaenda kuangalia namna wanavyofanya kazi na kujua changamoto gani zinazikabili chama hicho na kwa upande wa kwa mkulima tutaona mkulima amenufaika vipi na mbolea ya ruzuku na changamoto zipi ili tuweze kushughulika nazo ili mkulima aweze kunufaika na ile mbolea ya ruzuku.
"wakulima tunawashauri wajiunge kwenye AMCOS, wale ambao hawajajiunga kwenye AMCOS wajiunge ili waweze kutambilika kwenye umoja wa wakulima wa tumbaku duniani"
Alisema kuwa pindi mkulima anapo jiunga na vyama hivyo atapa fulsa ya kupata mikopo ya mbolea ili kuweza kulima kilimo bora na cha kisasa katika zao hilo.
"nafanyakazi ya ufatiliaji wa pembejeo za ruzuku hasa kwenye mbolea ya Ruzuku ya tumbaku"
Tumaini Lupola Meneja Mkuu wa Iringa Farmes Co operative Union alisema kuwa wametembelewa na timu kutoka wizara ya kilimo ambao wanafatilia mwenendo wa namna ambayo mbolea ya ruzuku la zao la tumbaku ilivyosambazwa na jinsi zilivyo wanufaisha wakulima.
"kwa Iringa Farmers Co operative union tunachochama kimoja ambacho ambacho tumejiunga mwaka jana na tumenufaika na mbolea za ruzuku"
Alisema kuwa timu hiyo itafika kwa wakulima ili kuweza kuangalia wakulima walivyonufaika na mbolea.
"nachoweza kusema mbolea ya NPK kwa ajili ya tumbaku ni gharama kubwa inauzwa zaidi ya 150,000/= lakini kupitia ruzuku hii wakulima wanapewa uwezo wa kuweza kununua hizi mbolea kwa bei ya chini
kwa sababu serikali inamchangia mkulima ili aweze kununua mbolea hiyo kwa bei nafuu,
kwa hiyo jambo hili litaleta matokeo chanya kwenye uzalishaji wa zao la tumbaku kwa maana kwamba wakulima wengi watafungua mashamba kwa ajili ya uzalishaji wa zao la tumbaku"
Aidha aliongeza kuwa wakulima wengi watapata utajiri kwa sababu gharama za uzalishaji zinashuka na gharama zinaposhuka mkulima anaongeza kipato.
Tumaini ameipongeza serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania kupitia Rais Samia Suluhu Hassan kwa sababu ameweka nguvu kubwa kuhakikisha sekta ya kilimo inainuka,tmeona mazao mengine serikali imeweka ruzuku katika kila mbolea kwenye tumbaku ndio ilikuwa ni zao pekee limebaki ambalo mbolea zake zilikuwa hazijaingizwa kwenye ruzuku lakini serikali imetathimini ikaona mahitaji ni makubwa ikaamua kuingiza na yenyewe kwenye ruzuku.
"Tunategemea kama uzalishaji ulivyoongezeka kwenye mazao mengine ya chakula ndio ikavyoenda kutokea kwenye zao la tumbaku,tunawashauri wakulima wetu wakae katika mkao wa kutumia fursa hii ambayo imeletwa na serikali ili waweze kunufaika na kilimo cha tumbaku"
0 Comments