Header Ads Widget

DR JAFO:WIZARA ZA KILIMO,UJENZI,VIWANDA NA BIASHARA ZITASHIRIKIANA KUTATUA CHANGAMOTO

Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE

Wakati Waziri wa viwanda na biashara  akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Njombe  baadhi ya wafanyabiashara wameitaka serikali kupunguza matuta ya barabarani pamoja na vituo vya ukaguzi ambavyo vimekuwa kikwazo kikubwa katika biashara.

Mbele ya Waziri huyo baadhi ya wafanyabiashara akiwemo   Zacharia Chaula Benadetha Sanga,Mhema Oraph na Eloy Mbilinyi  Wamesema wingi wa matuta barabarani yanapoteza muda mwingi katika kusafirisha mizigo pamoja na vituo vya ukaguzi ambavyo vimekuwa vikichelewesha shughuli za kibiashara.

Wengine wamesema vituo vingi vya ukaguzi wa  Magari watendaji wake Wamekuwa kikwazo kwani wanaendekeza Rushwa kupitisha Magari ya mizigo jambo ambalo linakatisha Tamaa ya kuendelea na biashara.

Awali mkuu wa mkoa wa Njombe Mhe.Antony Mtaka amesema baadhi ya changamoto zikiwemo za kwenye vituo vya ukaguzi alielekeza kupunguza vikwazo kwenye baadhi ya mizigo hasa mazao ya kuoza ili kunusuru hasara anayoweza kupata mfanyabiashara na Serikali yenyewe.

Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyabiashara mkoa wa Njombe Siphael Msigala amesisitiza suala la kupunguza Mlundikano wa Kodi kwenye biashara Moja ili kuondoka malalamiko ya miaka mingi.

Akijibu Hoja za wafanyabiashara mbalimbali Waziri wa viwanda na biashara Dokta Seleman Jafo amesema Wizara yake inaendelea kushughulikia changamoto hizo huku akiahidi kwenda kushirikisha Wizara nyingine katika kuweka Biashara katika mstaari Mnyoofu.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI