Na Josea Sinkala, Mbarali Mbeya.
Katika kuelekea maadhimisho ya miaka 48 tangu kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wanawake wa Chama wa Chama hicho (UWT), wamejitokeza kufanya usafi katika kituo cha afya Rujewa wilayani Mbarali mkoani Mbeya ili kuweka mazingira safi ya kutolea huduma za afya kwa wagonjwa na wananchi kwa ujumla.
Akizungumza kwenye zoezi hilo la kufanya usafi mmoja wa wanachama wa CCM ambaye ni mkazi wa mtaa wa Mbuyuni kata ya Rujewa
Rose Kinyaga, amesema wanamuunga mkono Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kufanya usafi katika maeneo ya hospitali na vituo vya afya ikiwa ni sehemu ya kaudhimisha miaka 48 ya kuwepo kwa chama hicho na kwamba mambo mengi yamefanywa na Serikali ikiwemo kwenye sekta za afya, elimu, barabara na nishati ya umeme.
"Hii siku kwetu ni maalum kabisa, tumetoka wanawake kufanya usafi hapa kituo cha afya Rujewa kwa maana ametujengea hospitali nzuri (Rais Samia Suluhu Hassan) na watumishi bora hivyo lazima tumuunge mkono tunaposherekea miaka 48 ya Chama chetu (CCM)", amesema Kinyaga.
Katibu wa jumuiya ya wanawake wa CCM kata ya Rujewa Anna Mgonzi, amesema katika kuadhimisha miaka 48, ya kuzaliwa kwa CCM wanakwenda na Rais Samia Suluhu Hassan kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 kutokana na kazi kubwa anazofanya ikiwemo kupunguza vifo vya mama na mtoto kwa wilaya hiyo.
"Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi kwa ujumla tumejitokeza kuja kufanya usafi katika kituo cha afya kata ya Rujewa, tumeona tuje tufanye usafi hapa ili kuweka mazingira safi na usalama wa kituo chetu cha afya ambacho kimekuwa msaada mkubwa kwa wananchi", amesema Anna.
0 Comments