Header Ads Widget

WANANCHI ROMBO WARIDHISHWA NA UTENDAJI KAZI WA PROF. ADOLF MKENDA NA DKT. SAMIA SULUHU HASSAN.

 


NA WILLIUM PAUL, ROMBO. 


WANANCHI wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro wamempongeza Mbunge wa jimbo la Rombo, Prof. Adolf Mkenda na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa waliyoifanya ya kufungua jimbo hilo kimaendeleo. 



Wakionyesha furaha yao katika maadhimisho ya sherehe za miaka 48 ya kuzaliwa kwa chama cha Mapinduzi katika viwanja vya shule ya Sekondari ya Mashati kata ya Katangara mrere ambapo mgeni rasmi alikuwa Mjumbe wa Kamati kuu na Katibu wa Nec Siasa na Uhusiano wa Kimataifa kupitia ccm, Rabia Hamid. 



Veronika Shirima mkazi wa kata ya Makiidi alisema kuwa, toka kuingia kwa Mbunge Prof. Adolf Mkenda wameshuhudia miradi mikubwa ya maendeleo ikipelekwa katika maeneo yao na kupeleka huduma za kijamii kusogea karibu ziadi nao.


"Mwaka 2015 tulichagua Mbunge kutoka chama cha upinzani tukijua angeweza kutuletea maendeleo lakini hatukuona chochote alichokifanya lakini kwa sasa ni muda mchache tangu tumchague Prof. Mkenda na tumeshuhudia mambo makubwa kwetu huyu kiongozi nakuhakikishia hana mpinzani" Alisema Veronika. 



Naye Ramadhani Saidi mkazi wa Tarakea alisema kuwa, kwa sasa wanajivunia mambo makubwa ambayo yametekelezwa na serikali ya awamu ya sita ikiwemo miundombinu ya barabara. 


"Tulikuwa na barabara ya chini kutokea Holili mpaka Tarakea na kila mwaka wabunge walishindwa kuipambania hii barabara kuwekwa lami lakini Prof. Mkenda ameonyesha kwa vitendo tumeshuhudia barabara hii imeanza kuwekwa lami Mwenyezi Mungu atupe nini sisi wanarombo" Alisema Saidi. 



Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya ya Rombo, Raymond Mangwala alisema kuwa, katika kipindi cha miaka mitatu ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wilaya hiyo imepokea fedha nyingi kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta za Afya, elimu, barabara, maji.


Mangwala alisema kuwa, jukumu la wananchi kwa sasa ni kuilinda miradi hiyo ili iweze kudumu muda mrefu na lengo lililokusudiwa na serikali liweze kutimia. 


Mwisho..

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI