Header Ads Widget

TAKUKURU PWANI YADHIBITI UVUJAJI WA MAPATO MAKUSANYO YAONGEZEKA.


 UDHIBITI wa upotevu wa mapato kwenye kizuizi cha Maliasili Wilaya ya Kibiti uliofanywa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Pwani umezaa matunda kwa mapato kuongezeka.

Aidha mapato ya makusanyo yameongezeka kutoka kiasi cha shilingi milioni 4.6 hadi 12 kwa wiki kwenye kizuizi hicho.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Pwani Alli Sadiki alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake juu ya mafanikio yaliyopatikana kipindi cha miezi mitatu iliyopita kuanzia Oktoba hadi Disemba mwaka 2024.

Amesema kuwa Takukuru ilisimamia ukusanyaji kuanzia Novemba 5 mwaka 2024 hadi Novemba 11 mwaka huo kwa saa 24 na kufanikiwa kukusanya kiasi hicho cha shilingi milioni 12  badala ya shilingi milioni 4.6 kwa wiki moja.

Aidha katika kipindi hicho walifanya ufuatiliaji wa miradi 52 ya maendeleo yenye thamani ya shilingi bilioni 12 ambapo hakukuwa na mapungufu huku mingine ikiwa inaendelea na utekelezaji sekta za afya, elimu, maji, barabara na katika uelimishaji umma wamefanya semina, mikutano ya hadhara, vipindi vya redio, kuimarisha klabu za wapinga rushwa na Takukuru Rafiki ambapo wamezifikia kata 11.

Ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa huo kuendelea kuunga mkono jitihada za mapambano dhidi ya rushwa kwa kuwafichua wale wanaoshiriki vitendo vya rushwa

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI