Header Ads Widget

SERA MP YA YA ELIMU NA MAFUNZO KUZINDULIWA JANUARI 31,2025

Na Hamida Ramadhan, Matukio Daima App                                   Dodoma

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, amesema kuwa maono ya Rais Tanzania Dkt, Samia Suluhu Hassan ni kuona na kuhakikisha vijana wa Kitanzania wanapomaliza shule wanakuwa na maarifa na ujuzi wa kutosha kwa ajili ya maisha yao ya baadae na maendeleo ya taifa kwa ujumla.

Hayo ameyasema leo Januari 29 jijini hapa wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelekea uzinduzi wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014, Toleo la 2023,

Amesema lengo la Rais Samia ni kuwaandaa wanafunzi kuwa mahiri katika kukabiliana na changamoto za kimaisha na kuendana na mahitaji ya dunia ya sasa. 

" Niukweli usiopingika Rais hakupendezwa na hali ya kuwa na wahitimu wa madaraja ya juu wasio na ujuzi wa uzalishaji, hali ambayo huwasababishia changamoto za ajira na maisha," amesema Msigwa.

Aidha kutokana na maono hayo, Rais Dkt, Samia alitoa maelekezo kwa serikali kuhakikisha elimu inalenga kuwajengea wanafunzi maarifa, mwelekeo chanya, maadili na ujuzi unaokidhi mahitaji ya kitaifa na kimataifa, ili waweze kushindana katika soko la ajira duniani.

Naye  pia, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo, amesema kuwa, maandalizi ya Sera pamoja na mkakati wa utekelezaji wake yamekamilika.

Ameeleza inafahamika wazi Sera ya elimu ndio mwongozo wa uendeshaji na utolewaji wa elimu nchini ambapo Mbali na Sera, Wizara imeandaa pia mkakati wa utekelezaji, ambao utawezesha kufanikisha malengo yake. 

Amesema kuwa Sera hiyo imeelekeza kuboresha mitaala ya elimu kuanzia ngazi ya awali, shule za msingi, sekondari, mafunzo ya ualimu na vyuo vikuu, ili kuhakikisha elimu inayotolewa inawapa wahitimu ujuzi unaohitajika katika soko la ajira na maisha kwa ujumla.

"Uzinduzi  huu wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014, Toleo la 2023 unatarajiwa kuwa hatua muhimu katika mageuzi ya elimu nchini, ukilenga kuleta mabadiliko chanya kwa kizazi cha sasa na kijacho, " Amesema Prof.Nombo

Hata hivyo Katika uzinduzi huo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuzindua  tarehe 31 Januari 2025, jijini Dodoma.



 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI