Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile amefanya ziara katika kiwanda cha Airplane Africa Limited (AAL) kinachotengeneza Ndege ndogo aina ya Skyleader 600 Mkoani Morogoro.
Kiwanda hiki kilianza kazi rasmi mwaka 2024 na hadi January 2025 kimeshatengeneza ndege tano ambazo zina uwezo wa kubeba abiria wawili.
Uwekezaji wa Kampuni hiyo kutoka Jamhuri ya Czech umechangiwa na juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan chini ya falsafa ya 4R.
Hata hivyo nchi pekee inayo yenye teknolojia kama hii ni South Africa pamoja na sisi Tanzania hivyo unaweza kuona vile nchi yetu inavyozidi kupiga atua katika maendeleo.
Ndege hizo ndogo kwa sasa zinaweza kutumika kwa kufanya tafiti, kilimo, ulinzi pamoja na utalii.
0 Comments