Header Ads Widget

RAIS DK.SAMIA ACHANGIA MILIONI 5O KUSAIDIA UJE ZI MSIKITI WA TAQWA SINGIDA

 

Na Thobias Mwanakatwe,Singida 

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan ametekeleza ahadi yake ya kutoa Sh.Milioni 50 kwa  ajili ya ujenzi wa msikiti wa Taqwa ambayo aliitoa kupitia kwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa, Ally Hapi.

Katibu wa Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Mkoa wa Singida, Omari Muna, alikabidhi hundi ya malipo ya fedha hizo jana kwa Sheikh wa Mkoa wa Singida, Issa Nassoro hafla iliyoshudiwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego na waumini, ambayo alitumiwa na Hapi.


Hapi akizungumza kwa njia ya simu alisema Rais amekuwa akisaidia mara kwa mara ujenzi wa misikiti na makanisa kutokana na mapenzi makubwa aliyonayo kwa Watanzania hivyo wananchi warudishe shukrani kwake kwa kuendelea kumuombea.

Alisema fedha hizo zitumike vizuri kwa malengo yaliyokusudiwa ili rais na  wadau wengine wanapoona kazi imefanyika vizuri waone umuhimu wa kuendelea kutoa zaidia kwa ajili ya ujenzi wa msikiti huo.

  Niwaombe tuendelee kumuombea dua na afya njema rais wetu kwani mambo anayoyafanya ni kutokana na mapenzi makubwa aliyokuwa nayo kwa Watanzania na ninampongeza Sheikh wa mkoa kwa kuwashirikisha waumini katika suala hili la ujenzi wa msikiti,” alisema.

Naye Sheikh wa Mkoa wa Singida, Nassoro, alimshukru Rais Dk.Samia kwa mchango wake huo na kuwataka wananchi kuendelea kumuunga mkono rais kutokana na mambo makubwa ya maendeleo anayoyafanya katika nchi yetu.


Alisema wapo baadhi watu wamekuwa na tabia ya kubeza mambo mazuri ya maendeleo yanayofanya rais na kwamba wananchi wasiwasikilize watu wa namna hiyo kwani kwa kipindi kifupi rais ameleta maendeleo makubwa nchini.

“Wapo baadhi ya wanasiasa walianza kuleta maneno maneno baada ya rais kuanza kuchangia kwenye misikiti na makanisa wakasema anatoa rsuhwa kwenye nyumba za ibada wanashindwa kuelewa kwamba rais anachangia kama ambavyo wanafanya watu wengine,” alisema.

Nassoro alisema katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025 wananchi waendelea kudumisha amani na upendo kama ilivyoasisiwa na waasisi wa Taifa hili.

“ Mwaka 2025 tunaenda kwenye uchaguzi, tutazame kuchagua viongozi waadilifu kama alivyo Rais Dk. Samia Suluhu Hassan,”alisema Sheik Nassoro.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dendego, alimshukru Rais Dk. Samia kwa mchango huo wa ujenzi wa msikiti ambapo alimuunga mkono na yeye (RC) kwa kuchangia Sh. Milioni 5.

“Tunawaskuru wale wote walioguswa katika kuchangia ujenzi wa msikiti huu ambapo zimefikia jumla Sh.milioni 176 na kila mmoja aliyeguswa apate baraka za Mungu,” alisema.


Hata hivyo, alisema malengo ya ujenzi huu bado hayajafikiwa hivyo waislam na wadau wengine waendelee kuunga mkono kwa kuiafuta pesa hasa ikizingatia msikiti huu upo katikati ya mji wa Singida hivyo ni lazima uonekane wa kisasa.

Naye Katibu wa BAKWATA Mkoa wa Singida, Muna alisema baada ya kuleta Singida atahakikisha miradi yote inayoetekelezwa inakwenda vizuri ikiwa ni pamoja na kuwaunganisha waislamu wote wa mkoa huu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI