Header Ads Widget

MISA TAN NA PACJI YASAINI MAKUBALIANO HAYA

Na. Matukio Daima media 

Dodoma

Taasisi ya Vyombo vya habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA Tan)  imesaini makubaliano na  Taasisi ya Pan Africanism Constructive Journalism (PACJI) ili kuwajengea uwezo wanachama wa MISA Tan.

Makubaliano haya yatagusa maeneo yafuatayo, kujengea uwezo wanachama wa MISA Tan kwenye kuandika habari jengefu, kuwa na programu za kubadilisha uzoefu baina ya wanachama wa MISA Tan na matawi ya nje ya Nchi ya PACJI, Kufanya tafiti Kwa pamoja na kushiriki kwenye mikutano ya kinataifa Kwa lengo la kusambaza falsafa ya uandishi wa habari jengefu 

Kwa upande wa MISA Tan aliyesaini makubaliano hayo ni Mwenyekiti wa MISA Tan Bwana Edwin Soko na Kwa upande wa Taasisi ya PACJI aliyesaini ni Daktari David Mrisho, pia makubaliano hayo ni ya miaka mitatu  yanayolenga kuzinufaisha Taasisi zote mbili ambayo yamefanyika kwenye hotel ya Royal Village Jijini Dodoma.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI