Header Ads Widget

PROF LIPUMBA AMUOMBA RAIS DKT SAMIA KUSIMAMIA 4R KUIMARISHA DEMOKRASIA

 


Na Fatma Ally Matukio DaimaApp, Dar 

Kwa mara ya kwanza Baraza kuu la Chama Cha wananchi CUF leo limeketi jijini Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine limejadili namna ya upatikanaji wa katiba mpya yenye maoni ya wananchi itakayokidhi mahitaji ya wananchi.


Akifungua kikao cha baraza hilo, Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) Taifa Profesa Ibrahim Lipumba amesema ni muhimu kupatikana kwa katiba mpya itakayotoa muongozo wa kusimamia namna ya kuindesha nchi ili kuwepo kwa upatikanaji wa haki.


 Aidha, amesema kuwa demokrasia imeporomoka nchini kote huku Tanzania ikidhihirika mwaka 2019  wakati wa uchaguzi wa Serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 huku akimuomba Rais Dkt Samia kusimamia 4r ili kuleta usawa.



Prof.Lipumba amesema  kuwa jukumu la kulinda Demokrasia nchini Tanzania ni la watanzania wote, hivyo ni vyema kuwajibika kwa  kila mmoja.


Aidha amesema, Rais Dkt Samia Suluhu Hassan anajukumu la kuhakikisha dosari zilizojitokeza katika uchaguzi huo wa 2024 na 2020 hazijitokezi tena katika uchaguzi mkuu unaofanyika Mwaka huu Nchini humo.


"Hali ya Demokrasia Duniani ilikua ikiporomoka ,wataalamu wa mambo ya Demokrasia wanaonesha katika tafiti tangu Mwaka 2006 ,Demokrasia imekua ikiporomoka Duniani"amesema  Prof.Lipumba


Nakuongeza kuwa ,hata Marekani ambapo pamoja na mapungufu mengi ndiko utaratibu wa Demokrasia ulipoanza kwa kuweza kuchagua viongozi wa kuwawakilisha wananchi nako Demokrasia imekua ikiporomoka."


Aidha ameongeza kuwa hata uchaguzi uliopita wa Marekani wa kumchagua Rais Donald Trump ambaye Mwaka 2020 aliyakataa matokeo ya uchaguzi inaonesha namna Demokrasia ilivyoporomoka nchini humo.


Ameongeza kuwa jukumu la ujenzi wa Demokrasia hapa nchini nila Watanzania wote,nakusisitiza kuwa Demokrasia imekua ikiporomoka.


Profesa Lipumba amedai kwamba kutokakana na kuonekana  kuporomoka Demokrasia nchini,amemuomba Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan  kusimamia ipasavyo falsafa yake ya 4R ili kuendelea kuimarisha Demokrasia nchini.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI