Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Wakati serikali ya mkoa wa Njombe ikikiri kuwapo kwa wazalishaji wa Mbegu na Miche ya Parachichi ya Kutosha Changamoto ya kukosekana kwa nishati ya umeme kwenye mashamba ya parachichi imetajwa kukwamisha uzalishaji kutokana na kukosa maji ya uhakika yanayotegemewa kuvutwa mabondeni kwa kutumia mashine.
Aidha wakulima wa zao Hilo mkoani Njombe mbali na kuzalisha Miche ya kisasa na yenye ubora mkubwa Inayotegemewa na mataifa mengine lakini Bado baadhi ya watanzania wanatajwa kuagiza mbegu ya tunda Hilo nje ya nchi jambo ambalo linafifisha jitihada katika sekta ya Kilimo.
Baadhi ya wakulima hao akiwemo Steven Mlimbila na Eligius Wella maarufu kama Madebe Wanasema pamoja na jitihada na mtaji mkubwa waliowekeza katika mashamba ya parachichi huko kifanya lakini nishati ya umeme imekuwa kikwazo na hivyo kuwafanya kukosa maji ya uhakika wakati wa kiangazi.
Mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka ametembelea mashamba ya wakulima hao kuona uzalishaji wa Miche ya parachichi ambapo amewataka Watanzania kutambua kuwa mkoa wa Njombe umewekeza kwenye ubora wa miche na mbegu za mazao mbalimbali hivyo hakuna sababu ya kuhangaika kuagiza nje ya Nchi.
Hata hivyo Mtaka amekiri kupokea changamoto ya kukosekana kwa nishati ya Umeme inayowakwamisha wakulima hao na kwamba atakwenda kuifanyia kazi.
Kwa mujibu wa Ofisa Kilimo mkoa wa Njombe Wilson Joel amesema Jumla ya Miche Milioni 1.5 inazalishwa kwa msimu Mmoja mkoani Njombe na hivyo fursa ni kubwa.
Kwa upande wake Ofisa Biashara mkoa wa Njombe Lusungu Mbede amesisitiza ubora katika uzalishaji wa Miche na parachichi zenyewe ili ziweze kukubalika katika masoko yote duniani.
Mataifa ya Burundi na Congo yameripotiwa kufika kununua Miche ya parachichi mkoani Njombe kutokana na Ubora mkubwa uliopo na hivyo Watanzania wametakiwa kuachana na biashara ya Kuagiza Miche nje ya Nchi.
0 Comments