Header Ads Widget

MBEYA CEMENT WAKABIDHI SAMANI SEKONDARI, DC APOKEA.

 

Na Matukio Daima media 

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mhe. Beno Malisa, amepokea mifuko 200 ya saruji kutoka kiwanda cha saruji Mbeya kwa ajili ya shule ya Sekondari Usongwe ikiwa ni sehemu ya kuchangia ujenzi wa bwalo la chakula unaoendelea kujengwa shuleni mjini Mbalizi.


Pamoja na mchango huo wa wadau, mkuu huyo pia amepokea viti na meza 220 kwa ajili ya shule ya Sekondari Songwe vilivyotolewa na Kampuni ya Saruji (Mbeya cement).



Mhe. Mkuu wa wilaya ya Mbeya Beno M. Malisa amekabidhi vifaa hivyo kwa uongozi wa shule hizo mbili za sekondari na kuwasisitiza utunzaji wa viti na meza ili viweze kutumika kwa muda mrefu.


Pia amewataka wazazi kuendelea kuwahimiza watoto wao kusoma ikiwemo kuwapeleka shule watoto wote ambao wamechaguliwa kuanza kidato cha kwanza mwaka 2025 na bado hawajaripoti shuleni.

 


"Mtoto ili aweze kusoma vizuri, anatakiwa kuwa ameshiba hivyo ni wajibu wetu wazazi na walezi kuchangia chakula shuleni lakini pia tuhakikishe watoto wote waliochaguliwa kujiunga na sekondari waende kwani Serikali imeweka mazingira sawa kwenye shule zetu", ameeleza DC Malisa.


Pia amewashukuru Kiwanda cha Saruji (Mbeya Cement) kwa kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuboresha miundombinu hasa kwenye sekta ya Elimu hapa nchini.


Kwa upande wake Diwani wa kata ya Bonde la Songwe Mhe. Michael Ngailo, amewashukuru wadau hao kwa kuunga mkono juhudi za Serikali kuboresha miundombinu katika shule yake ya sekondari na kwamba wamekuwa wakishirikiana nao katika miradi mbalimbali ya maendeleo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI