Na Matukio Daima media
Leo ni kumbukizi muhimu ya kuzaliwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa Dkt Linda Selekwa, ambaye amekuwa kiungo muhimu katika maendeleo ya kijamii na kielimu katika wilaya hiyo.
Dkt Selekwa, kwa miaka kadhaa, amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha jamii inapata mwamko juu ya umuhimu wa elimu, hususan kwa mtoto wa kike, suala ambalo limekuwa changamoto kubwa kwa familia nyingi za vijijini.
Katika kumbukizi hii, Dkt Selekwa ameendelea kutoa wito kwa wazazi na walezi kuwekeza katika elimu ya watoto wao, hasa watoto wa kike, ambao mara nyingi hukosa fursa za elimu kutokana na mila, desturi, na changamoto za kiuchumi. Alisema,
“Hakuna zawadi kubwa ambayo mzazi anaweza kumpa mtoto wake zaidi ya elimu. Mtoto wa kike mwenye elimu ni hazina kubwa kwa familia, jamii, na taifa kwa ujumla.”
Wilaya ya Mufindi, kama ilivyo kwa maeneo mengine ya vijijini, elimu zaidi inapaswa kuendelea kutolewa kwa jamii ili kutoa msukumo wa elimu kwa watoto wa kike, ikiwa ni pamoja na kuendelea kukemea ndoa za utotoni, mimba za mapema, na ukosefu wa mwamko wa wazazi kuhusu umuhimu wa elimu jambo ambalo Dkt Selekwa amekuwa akishirikiana na viongozi wa kijamii, walimu, na asasi za kiraia ili kupambana na changamoto hizi kwa kuelimisha jamii kupitia mikutano, semina, na programu za uhamasishaji.
Dkt Selekwa amekuwa akihimiza wazazi kwani ni jukumu la kila mzazi kuhakikisha watoto wote wanapata haki yao ya msingi ya elimu bila kujali jinsia.
“Tunahitaji kubadilisha mtazamo wa kijamii. Mtoto wa kike ana haki sawa ya kupata elimu kama mtoto wa kiume. Elimu inafungua milango ya fursa na kumwezesha mtoto wa kike kuchangia maendeleo ya familia na jamii kwa ujumla,” alisema.
Hivyo ni wazi wakati Leo anasherekea kumbukizi yake ya kuzaliwa jamii ni Mufindi inatambua fika jitihada zake katika kumwakilisha Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ndani ya Mufindi .
Dkt Selekwa anawapongeza wazazi na walezi ambao tayari wameonyesha dhamira ya dhati ya kusomesha watoto wao.
Ikumbukwe kuwa mafanikio mengi yaliyopatikana Mufindi yanatokana na juhudi za pamoja kati ya serikali na wananchi wenyewe.
Wapo mabinti waliokatishwa masomo KWA kupata mimba na sasa kupitia Mradi wa Youth Angency Mufindi (YAM) na Mradi wa Rural Development Organization (RDO) mabinti wake wanampongeza sana mkuu huyu wa wilaya kwani amekuwa mfariji Wao wa kweli .
Hawa ni mfano hai wa kile kinachoweza kupatikana endapo kila mtoto wa kike atapewa nafasi ya kusoma.
“Leo nina ndoto kubwa za kuwa daktari kwa sababu wazazi wangu walinipa nafasi ya kwenda shule,” alisema mmoja wa wanafunzi waliotoa ushuhuda kutoka YAM na RDO
Huu ni ushahidi tosha kuwa Mheshimiwa Dkt Linda Selekwa ni chacho kwao .
Ifahamike kuwa kuwa serikali ya Wilaya ya Mufindi itaendelea kusimamia kwa ukamilifu suala la elimu, hususan kwa mtoto wa kike.
Kumbukizi hii ya kuzaliwa kwa DC wa Mufindi imekuwa sio tu fursa ya kusherehekea maisha na mafanikio yake binafsi, bali pia kuchochea ari mpya ya maendeleo katika jamii, hususan katika kupigania haki ya elimu kwa mtoto wa kike. Kauli mbiu ya hafla hii ni “Mtoto wa Kike na Elimu: Hazina ya Taifa.”
0 Comments