Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Zaidi ya shilingi bilioni mbili zimetajwa kuendelea kujenga vituo vya Afya katika Halmashauri ya mji wa Njombe ili kupunguza changamoto za Afya kwa wananchi huku Wizara ya Afya ikiendelea kupeleka Magari ya kubeba wagonjwa wa Dharura kwenye vituo hivyo.
Katika Hafla ya Makabidhiano ya gari la wagonjwa wa Dharura Ambulance kwenye kituo Cha Afya Ihalula kata ya Utalingolo Mbunge wa Jimbo la Njombe Mjini Deodatus Mwanyika amesema gari Hilo limetumia gharama kubwa kulinunua na kwamba uwekezaji huo unakwenda sambamba na uboreshwaji miundombinu ya kutolewa huduma za afya.
Diwani wa kata ya Utalingolo Erasto Mpete Ambaye ni mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Njombe amewataka wananchi kulitunza gari Hilo ili liwasaidie pamoja na vizazi vijavyo.
Awali mganga mfawidhi wa kituo Cha Afya Ihalula Dokta Happiness Kwilasa amesema ujio wa gari Hilo utasaidia kupunguza adha kwa wananchi ambao Wamekuwa wakitumia gharama kubwa kusafirisha wagonjwa pindi wanapopewa Rufaa.
Aidha Dokta Kwilasa amesema pamoja na ujio wa gari Hilo lakini Bado kituo kinakabiliwa na Changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa wataalamu na miundombinu hasa nyumba za kuishi.
Naye Dokta Jabil Juma mganga mkuu wa Halmashauri ya mji wa Njombe amesisitiza kutolewa Bure kwa huduma ya gari Hilo kwani ni jukumu la Serikali kugharamia huku akisema Tayari Magari matano yameshatolewa na yanafanyakazi.
Agnes Mbilinyi na Sebastian Fungilwa ni wakazi wa Ihalula kunako kituo Cha Afya ambao wanasema sasa watapata nafuu pindi wanapopatwa na Rufaa.
Diwani wa Kata ya Makowo Honolatus Mgaya anasema Kituo chake Cha Afya Makowo kilipata gari yapata mwaka Sasa lakini uendeshaji wake unategemea mapato ya Kituo hicho.
Kwa mujibu wa Mganga mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Njombe hadi sasa Halmashauri imepata magari matano ya Wagonjwa wa Dharura kwenye vituo vya Afya Vinne na Moja la Hospitali.
0 Comments