Header Ads Widget

KIGOMA YATOA GARI, PIKIPIKI KWA HALMASHAURI KUIMARISHA CHANJO YA MAGONJWA KWA WATOTO

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

MKUU wa mkoa  Kigoma Thobias Andengenye amekabidhi gari moja la kutolewa chanjo kwa timu ya uendeshaji afya ya mkoa sambamba na pikipiki 12 kwa halmashauri nane za mkoa huo ili kufanikisha zoezi la utoaji chanjo kwa Watoto.

Andengenye amekabidhi gari hilo kwa Kaimu Katibu Tawala wa mkoa Kigoma sambamba na kukabidhi pikipiki kwa Mkuu wa wilaya Kigoma, Rashid Chuachua ambaye aliwawakilisha wakuu wa wilaya sita katika halmashauri nane za mkoa Kigoma.

Akizungumza katika kukabidhi pikipiki Mkuu huyo wa mkoa Kigoma alisema kuwa mkoa huo umepiga hatua kubwa katika utoaji wa chanjo za aina mbalimbali kwa watoto kuanzia siku moja hadi miaka mitano ambapo utoaji huo wa chanjo umefanikisha kudhibiti magonjwa mbalimbali kwa Watoto.

Alisema kuwa mkoa Kigoma uko mpakani ukipakana na nchi za ukanda wa maziwa makuu ambazo zimekuwa zikikumbwa na milipuko ya magonjwa mbalimbali hivyo kuimarishwa kwa vitendea kazi hivyo vinaleta hakika ya chanjo kutolewa na kumfikia kila mtoto anayekusudiwa ambapo kwa sasa utoaji chanjo za magonjwa kwa watoto imefikia asilimia 95.

Awali Mganga Mkuu wa mkoa Kigoma Damas Kayera alisema kuwa Pamoja na mafanikio ambayo mkoa umepata katika utoaji wa chanjo mbalimbali mkoani humo ikiwemo polio, surau, rubela na nyingine nyingi na bado kazi ya ziada ilikuwa ikifanyika kuwafikia wananchi ambao wengine walikuwa mbali yenye miundo mbinu duni ya usafiri kufikika.

Hata hivyo alisema kuwa kuwepo kwa gari hiyo ya chanjo katika timu ya usimamizi wa chanjo ya mkoa itafanya chano kufika kila mahali kwa wakati lakini pia pikipiki 12 zilizotolewa zitafanikisha kuwafikia wananchi hadi maeneo ambayo hakuna usafiri na hivyo itauhakikishaia mkoa kuwa watoto wote watakuwa salama dhidi ya magonjwa.



 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI