Header Ads Widget

CHIEF MKONGWA NA UKOO WAKE WATEMBELEA WATOTO YATIMA KUUANZA MWAKA MPYA WA 2025

 

Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE

Mwaka mpya wa 2025 umetakiwa kutumika vizuri kwa kutenda matendo mema na ya huruma kwa Yatima na makundi maalumu ili kujipatia thawabu kwa mungu.

Watoto Yatima na wanaoishi katika mazingira magumu na hatarishi ni miongoni mwa makundi ya kutazamwa kwa karibu kauli iliyotolewa na Chief wa Kabila la Wabena Mzee Charles Mkongwa wakati wa zoezi la utoaji misaada kwa watoto wanaoishi katika kituo cha kulelea watoto cha Compassion Foundation COF Kilichopo mjini Njombe.



Chief huyo  akiambatana na Ukoo wake wa akina Mkongwa waliokutana pamoja kujadili masuala mbalimbali katika kuuanza mwaka mpya wametembelea kituo hicho na kutoa misaada mbalimbali huku akiwasisitiza watoto hao kutii wanayofundishwa.

Sister Lusia Mlowe ni Mkurugenzi wa Kituo cha COF ambaye ameushukuru ukoo wa akina Mkongwa Kwa misaada hiyo ambao wamekuwa wakifika kila mwaka katika kituo hicho na kuwapa misaada watoto  wanaolelewa kituoni hapo huku Sister Sesilia Sasi akisema hadi sasa Kuna watoto 32 wenye changamoto tofauti.

Naye mwenyekiti wa Taifa wa Ukoo wa Mkongwa Royal Family Bwana Albert Mkongwa amesema wamepeleka zawadi mbalimbali kwa watoto hao zikiwemo sabuni na Fedha ili kuwaunga mkono kwani ni muhimu kuwaunga mkono watoto wanaopitia madhira mbalimbali.



France Mgimba ni miongoni mwa Watoto waliopo katika Kituo cha COF Ambaye anashukuru kwa kupatiwa misaada hiyo kwani mazingira wanayoishi yanawafanya kukosa furaha pindi wanapokosa mahitaji muhimu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI