Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Chama Cha mapinduzi CCM mkoa wa Njombe kimepiga marufuku wanachama wa chama hicho kujipitisha na kutoa zawadi,misaada au kitu chochote katika kipindi hiki bila kuridhiwa na vikao halali vya chama na kwamba hatua Kali za kinidhamu zitachukuliwa kwa atakayebainika.
Kupitia maazimio ya Kikao Cha Halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Njombe katibu wa siasa uenezi na mafunzo Josaya Luoga amesema kwa Mwaka huu wa 2025 hakuna atakayejipitisha na kutoa msaada au zawadi yoyote kwa wananchi au wapiga kura na kuachwa salama kwani hizo ni hujuma dhidi ya waliopo mamlakani katika kata na Majimbo.
Aidha Luoga amesema Chama hicho kimepiga marufuku tabia za baadhi ya vijana kujirekodi au kutumia vyombo vya habari kuwakaribisha wagombea kwenye kata au Majimbo ili hali muda wa Uchaguzi bado kwani ni kukiuka kanuni za Chama.
Amesema Kuna tabia za baadhi ya vijana kuanza kukaribisha wagombea ili hali Bado Kuna madiwani na wabunge wanaoendelea kufanyakazi Hadi hapo watakapomaliza muda wao.
Hata hivyo Chama Cha mapinduzi CCM mkoa wa Njombe kimewatakia kila lenye heri wanachama na wananchi wote katika Mwaka mpya wa 2025 huku kikiwataka kudumisha amani na kushiriki katika uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura katika zoezi linalotarajia kuanza Januari 12 Hadi 18 Mwaka huu.
0 Comments