Header Ads Widget

JAMILA MIYONGA WA UWT KILOSA ARUDISHA TABASAMU KWA MLEMAVU ALIYEKAA NDANI KWA MUDA MREFU BILA KUTOKA

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wanawake ya Chama cha Mapinduzi,UWT, Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro ,Bi Jamillah Miyonga ameitumia Sikukuu ya mwaka mpya kurejesha Tabasamu kwa mwanamke mwenye ulemavu wa kupooza wa miguu Bi Salome Bernard mkazi wa Rudewa wilayani humo, baada ya kukaa ndani kwa muda mrefu bila kutoka kwa kukosa mahitaji muhimu ya kibinadamu.


Mwenyekiti Miyonga amemkabidhi mwanamke Bi Salome zawadi mbalimbali ikiwemo Kiti mwendo cha matairi matatu kumuwezesha kutoka nje na pia kinatumika kama choo Ili kumrahisishia mahitaji yake mbalimbali , sambamba na Godoro, Mashuka na vitu vingine vya ndani.

Aidha ameshiriki na familia ya mwanamke huyo aliyekaa ndani kwa zaidi ya miaka25, akilala ndani bila kutoka nje, huku shughuli zake zote zikifanyika kitandani kwa kupika chakula cha mchana na kula pamoja nao.

Katika salamu zake za mwaka mpya, Mwenyekiti huyo alifikisha Salamu za Sikuku za Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Salamu za Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndg. Marry Chatanda kwa kubainisha kuwa viongozi hao wapo pamoja na watanzania wakiwemo watu wenye mahitaji maalum na wametoa salamu za pole kwa Bi Salome.

 

Miyonga akasema  viongozi hao wamekua mfano wa kuigwa kwa  kutoa miongozo mbalimbali hasa kwa viongozi wa chini yao kuwafikia wananchi katika makundi yote ya kwenye  jamii.

Akwasihi wananchi wa Kilosa na wadau wengine wa maendeleo kuwakumbuka watu wenye uhitaji kama Bi Salome kwani wako wengi na jukumu la kuwasaidia ni la kila mmoja.

Mwenyekiti Miyonga akatoa wito kwao kuwafariji kwa hali na mali watu wa aina hiyo kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wanatoa sadaka ya kudumu hata baada ya maisha ya Duniani.

Akawashauri wadau wengine watakaoguswa kusaidia wanawake wenye uhitaji katika Wilaya hiyo ya  Kilosa kuwasiliana na ofisi ya UWT ya wilaya hiyo ya Kilosa kwani bado wahitaji ni wengi na mahitaji yao ni makubwa.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI