Na Shemsa Mussa -Matukio Daima
Kagera.
Maambukizi ya Bungua mweusi yaendelea kulishambulia zao la kahawa Mkoani Kagera huku wananchi wakihofia kulipoteza zao Hilo
Afisa kilimo kutoka Halmashauri ya Bukoba Babylus Mashauri akiongea katika kikao cha baraza la madiwani amesema halimashauri hiyo imepata changamoto ya kisumbufu kinachoshambulia Zao la Kahawa kinaitwa Bungua mweusi wa Kahawa.
Mashauri amesema madhara yake ni kwenye matawi ya Kahawa anatoboa matundu madogo na kuingia ndani anataga mayai kwaajili ya kuzaa.
Amesema Bungua wa kiume anaweza kuishi siju 6 na Bungua wa kike anaishi siku 58 na ana uwezo wa kutaga mayai kati ya ( 20- 50 ) kwa uzao mmoja lakini baada ya kuanguliwa hao wadudu Bungua wa kike anakaa siku ( 19 ) kisha anaondoka kwenda kutafuta makazi mengine.
Amesema Athari za Bungua huyu ni kukauka kwa Matawi yaliyoshambuliwa na kadri anavyoendelea kushambulia athari inaweza kuwa kubwa kupelekea kupoteza uzalishaji kwa kiwango kinachoanzia asilimia ( 20- 50 ) ya uzalishaji wa Zao la Kahawa.
Anasema mikakati ya kukabiliana na ugonjwa huo ni pamoja na kuwajengea uwezo wa taalam wa kilimo kwa maana ya kuwatambua wadudu pamoja na madhara yake.
Amesema hatua ya pili ni kampeni kwaajili ya kumtokomeza mdudu huyo mwenye madhara makubwa kwa jamii inayojishughulisha na zao hilo kujiongezea kipato.
Anasema Zao la kahawa ndiyo kipaumbele kwa mkoa wa Kagera na ni Zao la kiuchumi na kudai kuwa wapo kwenye mapambano ambayo kimsingi ni ya kiuchumi kwa sababu Kahawa ndiyo uchumi wao.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Erasto Siima wakati akifanya mahojiano na vyombo mbalimbali baada ya kikao na Madiwani
amesema Tegemeo kubwa la mkoa na Wilaya ya Bukoba katika kukuza uchumi ni zao la Kahawa ambalo sasa umeibuka ugonjwa unaoshambulia mmea huyo.
" Hili jambo ikiendelea litashusha uchumk wetu, wataalam wa kilimo wameshasambaa maeneo yenye mashamba ya kahawa kuangalia namna ya kufanya utatuzi,Nimeagiza wataalam wa kilimo kuangalia hasa maeneo yaliyo na uhalibifu ili kuweza kushughulikia "anasema Mkuu wa wilaya hiyo.
Naye mwenyekiti wa Halmashauri ya Bukoba Murshid Ngeze ,amemuomba mkuu wa Wilaya kuwasaidia katika kukabiliana na tatizo la ugonjwa huo unaotishia maisha ya wakulima wa Kahawa.
Ngeze ,amewataka wataalam wa kilimo kutafuta suluhisho la haraka ili kudhibiti kabla ya tatizo kuwa kubw kwenye jamii.
0 Comments