Header Ads Widget

KATAVI WAKUBALI MBINU ZA NJOMBE KUKABILIANA NA LISHE


Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP Njombe

Serikali ya mkoa wa Katavi imekiri kwenda kuanzisha Kampeni maalumu ya Mapambano dhidi ya udumavu kama ulivyofanya mkoa wa Njombe ili kukabiliana na changamoto za lishe kwa watoto.

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mlindoko ametoa kauli hiyo akiwa mkoani Njombe kwenye ziara ya siku mbili kujifunza namna Kampeni ya Lishe ilivyofanikiwa na hii ni baada ya maelekezo ya Rais Samia kuutaka mkoa wa Katavi kwenda kujifunza Njombe.

Mlindoko amesema Tayari baadhi ya mambo walishaanza kuyafanyia kazi juu ya kukabiliana na Udumavu kwani vipo vyakula vya kila aina na mikoa hiyo inategemewa kwa uzalishaji wa mazao ya  Chakula katika Taifa hivyo ni lazima wakafanye kwa vitendo kwa kuelimisha jamii umuhimu wa kula mlo kamili.

Awali mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka amesema ushirikishi wa makundi mbalimbali katika jamii yalisaidia kufanikisha Kampeni ya lishe iliyosaidia kushuka kwa kiwango Cha udumavu.

Ofisa Lishe mkoa wa Katavi Suleiman Hamis amesema licha ya mkoa wao kuwa na Asilimia 32.2 ya Udumavu tofauti na Njombe yenye Asilimia 50.4 lakini wameona umuhimu kufika kujifunza namna Kampeni ilivyofanyika kwa maelekezo ya Rais.

Kwa upande wake Katibu tawala mkoa wa Njombe Bi.Judica Omary amesema baada ya Kampeni hiyo Walifanya utafiti wa ndani wa Hali ya Lishe na kubaini kushuka kwa kiwango Cha udumavu Toka Asilimia 50.4 Hadi 40.2

Baadhi ya wajumbe walioambatana katika ziara hiyo wamehoji maswali mbalimbali juu ya Utekelezaji wa Kampeni hiyo Ambayo imeonekana kuwa chachu kwa Taifa na mikoa yenye changamoto za Afya za Lishe.

Hadi Mwaka jana Takwimu zinaonesha kuwa kiwango cha udumavu kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano bado ni kikubwa ambapo kwa mkoa wa Kigoma ni 27.1%, Katavi 32.2%, Njombe 50.4%, Songwe 31.9% na Rukwa 49.8%.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI