Madereva bodaboda 153 wamehitimu mafunzo ya udereva na wahitimu wa udereva wa magari 17 katika Chuo cha VETA wilayani Buhigwe mkoani Kigoma ikiwa ni mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwa Chuo hicho wilayani humo.
Amesema hayo wakati akitoa taarifa ya hafla fupi ya Mahafari ya kwanza Wanafunzi wa ufundi stadi wa kozi mbalimbali katika Chuo cha VETA wilayani Buhigwe mkoani Kigoma Mkuu wa Chuo cha VETA Buhigwe Ally Bushiri.
Amesema kati ya wahitimu hao wa kozi ya udereva bodaboda ni 153, wamehitimu mafunzo ya udereva wa magari 17, muhitimu wa ujenzi mmoja, fundi bomba mmoja, na computa ni mmoja na Chuo Bado kinaendelea na mafunzo kama hayo katika Wilaya jirani zisizo na huduma ya vyuo vya VETA kama wilaya ya Uvinza.
Aidha alitaja aina za kozi fupi na ndefu zilizotolewa tangu kuanzishwa kwa Chuo hicho mwanzoni mwa mwaka 2024 kuwa ni pamoja na ufundi selemala, udereva wa bodaboda, udereva wa magari, kuchomea, computa, ujenzi, cherehani, udereva wa magari ya abiria.
Bushiri alisema VETA Buhigwe inakabiriwa na mwitikio mdogo wa wanabuhigwe ambapo wanaendelea kutoa elimu ya kuhamasisha jamii waje chuoni hapo wapate elimu ya ufundi stadi.
Mkuu wa wilaya ya Buhigwe Kanal Michael Ngayalina katika hotuba yake iliyowakirishwa na Afisa Tawala wilaya Buhigwe Emma Malilo amewataka Madereva bodaboda wilayani Buhigwe mkoani Kigoma wametakiwa kufichua waharifu na vitendo vya uharifu kuwafikisha kwenye vyombo vya dola ili hatua za kiusalama na za kisheria zichukuliwe dhidi ya waharifu hao.
Amesema Madereva bodaboda hao waliohitimu wapo Madereva bodaboda binafsi na maafisa usafirishaji wanaobeba abiria wa aina mbalimbali katika jamii.
"Na hao abiria wapo watu wema na wasio wema basi tushirikuane na Viongozi wa serikali tuweze kufichua yale maovu ambayo tutayajua au tutayasikia wakati wakubeba abiria hao"
"Wakati mwingine ubabeba mtu unajua kabisa anakwenda kuvamia sehemu fulani unaamua kunyamaza hautoi ushirikiano lakini naomba ukisikia jambo lolote utoe taarifa kwenye vyombo vya dola"
"Sio lazima ukatoe taarifa kwenye kijiwe kwa usalama wako peleka taarifa sehemu ambayo utakuwa salama zaidi" alisema Kanal Ngayalina.
Aidha amewataka kuzingatia kanuni, Sheria na taratibu za usalama barabarani na Sheria za nchi katika kuhudumia Wananchi ambazo ni kwa usalama wa abiria wanaowabeba na usalama wao binafsi.
0 Comments