Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Wakati baadhi ya wakulima wa Mahindi katika Kijiji Cha Kidugala Wilaya ya Wanging'ombe wakilalamikia mahindi yao kutoota vizuri Jeshi la Polisi mkoa wa Njombe limesema limewakamata watu watatu kwa tuhuma za kuuza Mbegua Feki katika Kijiji hicho.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Mahamoud Banga akizungumza na Vyombo vya Habari wakati akitoa Taarifa ya Utendaji kazi wa Jeshi la Polisi katika Kipindi cha Mwezi mmoja amesema watu hao wamekamatwa kwa tuhuma za Kuuza Mbegu feki zenye uzito wa Kg 286.
Kituo hiki kimezungumza na baadhi ya Wakulima mkoani Njombe akiwemo Pascal Yeremia ambao wanasema hatua ya kuuziwa mbegu feki kunawatia hasara na wanapaswa kufikishwa haraka kwenye vyombo vya sheria
Pasiems Chawala ni mtaalamu wa Kilimo ambaye kwa Njia ya Simu anasema kitendo cha wakulima kuuziwa mbegu feki kinaleta madhara mengi yakiwemo ya Kiuchumi.
Mara kadhaa mkoa wa Njombe umeripotiwa kukamatwa kwa Pembejeo feki pamoja na baadhi ya wafanyabiashara kujaza Mchanga kwenye Mifuko ya Mbolea na Mahindi jambo ambalo linawatatizo wakulima.
0 Comments